Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KUHUSU TAARIFA ZA KIFO CHA LETICIA NYERERE


Aliyekuwa Mbunge wa Viti Maalum kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Leticia Nyerere amefariki dunia katika hospitali ya Doctors Community iliyopo Lan ham, Maryland nchini Marekani jana saa mbili usiku kwa saa za Afrika Mashariki.

Leticia aliolewa kisha kutengana na mtoto wa Hayati Baba wa Taifa, Madaraka Nyerere mwaka 1996, ambapo walifanikiwa kupata watoto watatu.


Leticia alikuwa mtoto wa Mzee Musobi Mageni. Julai 27 2015, Leticia alitangaza kuihama CHADEMA na kurejea Chama Cha Mapinduzi (CCM).


Mungu ailaze roho ya Marehemu mahali pema peponi,
Amina.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com