NB-Picha haihusiani na habari hapa chini |
OFISA mtendaji wa kijiji cha Ulinji Manispaa ya Sumbawanga mkoani
Rukwa, Livinus Mbutu amemfikisha kituo cha polisi mkazi wa kijiji
hicho Martin Daud ( 28) akituhumiwa kumpa ujauzito dada yake mwenye
umri wa miaka (14) ambaye pia ni mwanafunzi wa darasa la saba.
Tukio hilo lilitokea Januari 18, majira ya saa 8;20 za mchana baada
ya mtuhumiwa huyo kukamatwa na mgambo wa kijiji kutokana na kuwa
alikuwa amejificha porini kwa siku tatu akikimbia mkono wa sheria
baada ya kufanya tukio hilo.
Akizungumza na malunde1 blog mtendaji Mbutu alisema kukamatwa kwa
mtuhumiwa huyo kulitokana na taarifa kutoka kwa walimu ambapo msichana
huyo alikuwa akisoma walitoa taarifa kuwa mwanafunzi huyo anaonekana
kuwa ni mjamzito.
Baada ya taarifa hizo wazazi wa msichana huyo wakiwa na mwalimu mkuu
pamoja na mtendaji huyo walikwenda kutoa taarifa kituo cha polisi na
kufungua kesi RB 297 na walipatiwa fomu ya matibabu (PF.3) kisha
kwenda katika zahanati ya kijiji kwaajili ya uchunguzi .
Baada ya uchunguzi ilibainika kuwa mwanafunzi huyo ana ujauzito wa
miezi minne na baada ya kuhojiwa alikiri kuwa kaka yake wa tumbo moja
ndiyo aliyempa ujauzito kutokana na kuwa walikuwa na uhusiano wa
kimapenzi kwa muda mrefu.
Naye baba wa watoto hao Oscar Marekani alisema kuwa kijana wake huyo
wa kiume alikuwa ameoa lakini aliachana na mke wake na kurudi nyumbani
ambapo aliendelea kuishi katika familia hiyo bila wao kujua kama
watoto wao wana uhusiano wa kimapenzi.
Alisema watoto hao walikuwa wakienda shambani kulima bustani ndipo
walikuwa wakikutana huko na kuhusiana kimapenzi hadi binti yake huyo
kupata ujauzito na kuficha lakini walimu ndiyo waliogundua hali hiyo.
Marekani alisema kuwa tukio hilo la kusikitisha limeitia aibu kubwa
familia yake na wameliachia jeshi la polisi lichukue hatua kutokana na
tukio hilo kwani wameshindwa kumvumilia Mtoto wao huyo kutokana na
kuwa hilo ni tukio la pili kwani miaka miwili iliyopita alimpa
ujauzito mtoto wa baba yake mkubwa.
Kwa upande wake mama wa watoto hao Cecilia Lupia alisema kuwa huo ni
mkosi katika familia yao na kamwe hata wasamehe watoto hao kwani
wamesababisha aibu kwa familia hiyo na yeye atakosa furaha kwa maisha
yake yote kijijini hapo.
Na Walter Mguluchuma-Malunde1 blogSumbawanga