Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Mkoani Katavi imemuhukumu Frank Jonas(27) Mkazi wa Mtaa wa Mpanda Hoteli kutumikia kifungo cha miaka 30 jela baada ya kupatikana na kosa la kutaka kumbaka hawala yake(Mpenzi wake) mwenye umri wa miaka(17) ambae jina lake limehifadhiwa Mkazi wa mtaa huo.
Hukumu hiyo ilitolewa juzi na Hakimu Mkazi mfawidhi wa Mahakama ya Wilaya ya Mpanda Chiganga Ntengwa na kuvuta hisia za watu wengi ambao walikuwa hawajui kufanya hivyo kuwa ni kosa.
Awali kabla ya kutolewa kwa hukumu hiyo mwendesha mashitaka Mwanasheria wa Serikali Ongela Malifimbo alidai kuwa mtuhumiwa alitenda kosa hilo January 9 mwaka huu muda wa saa nane mchana katika eneo la shule ya Sekondari Mwangaza.
Siku hiyo ya tukio mtuhumiwa alimvizia njiani msichana huyo wakati alipokuwa akipita katika eneo hilo na kisha alimtupia kwenye majani ambayo yalikuwa marefu.
Mwendesha mashitaka huyo aliendelea kuiambia Mahakama kuwa baada ya kuwa amemtupia kwenye nyasi alimvua kwa nguvu nguo zake na kisha alimlalia juu ya kifua chake na wakati huo msichana huyo alikuwa akipiga mayowe ya kuomba msaada .
Alieleza watu waliokuwa karibu na eneo hilo baada ya kuwa wamesikia mayowe ya kuomba msaada walifika kwenye eneo hilo na walimkuta Frank Jonas akiwa amemlalia kifuani msichana huyo huku akiwa anahangaika kutaka kumvua nguo yake ya ndani na wakati huo msichana akiwa anaendelea kupiga yowe ya kuomba msaada.
Watu walifika kwenye eneo walilazimika kumtoa kwa nguvu juu ya kifua cha msichana huyo huku mtuhumiwa akiwa anawasihi wamuachie kwani anamfanyia hivyo kwa vile ni hawara yake(Mpenzi) na alikuwa amekula hela zake hata hivyo walifanikiwa kumwondoa na kisha walimpeleka kwenye kituo cha polisi cha Mpanda huku akiwa haja timiza lengo lake la kufanya tendo la ndoa.
Mshitakiwa baada ya kusomewa mashitaka alikiri kutenda kosa hilo hapo January 9 mwaka huu katika eneo la Shule ya Sekondari Mwangaza.
Baada ya mshitakiwa kukiri kosa hilo Hakimu Chiganga Ntengwa alimweleza mshitakiwa kuwa kama inayosababu yoyote ya msingi inayoweza kuishawishi Mahakama impunguzie adhabu Mahakama inatoa nafasi hiyo kwa mshitakiwa kujitetea .
Mshitakiwa katika utetezi wake aliomba Mahakama impunguzie adhabu kwa kuwa alifanya hivyo kwa vile msichana huyo alikuwa ni mpenzi wake na alikuwa amekula fedha zake.
Maombi hayo yalipingwa na mwanasheria wa Serikali kwa kile alichodai kuwa hata kama alikuwa ni mpenzi wake hakutakiwa kutaka kufanya tendo la ndoa bila lidhaa ya msichana yule.
Hakimu Chiganga akisoma huku hiyo alisema mshitakiwa Frank Jonas Mahakama imemtia hatia kwa kosa la kifungu cha sheria 132(1) sura ya 16 cha marekebisho ya sheria ya mwaka 2002.
Kutokana na kosa hilo Mahakama imemuhukumu mshitakiwa kwenda jela kutumikia kifungo cha miaka 30 jela kuanzia juzi.
Na Walter Mguluchuma-Malunde1 blog Katavi
Social Plugin