Rais Magufuli amewasimamisha kazi Kamishna Mkuu wa uhamiaji Sylivester Ambokile na Kamishna wa Utawala na Fedha wa Uhamiaji Piniel Mgonja.
Magufuli amefikia uamuzi huo kutokana na dosari kadhaa zilizobainishwa na waziri wa mambo ya ndani Charles Kitwanga, alipotembelea katika ofisi za uhamiaji.
(PICHANI: Waziri wa mambo ya ndani akiongozana na Kamishna mkuu wa Uhamiaji, Sylivester Ambokile katika ziara yake hivi karibuni.
Katika hatua nyingin, Rais Magufuli amemrejesha kwenye kazi yake ya awali ya katibu tawala wa mkoa wa Manyara, Eliakimu Maswi kutokana na sababu za kitaaluma.
Hivi karibuni Maswi aliteuliwa kuwa Naibu Kamishna Mkuu wa TRA nafasi ambayo ameishika kwa muda usiozidi wiki 3, na sasa atarejea mkoani Manyara.
Social Plugin