MBWANA SAMATTA NI NOMAAA!! ANYAKUA TUZO YA MCHEZAJI BORA WA AFRIKA ANAYECHEZEA BARANI AFRIKA
الجمعة, يناير 08, 2016
Mwanasoka raia wa Tanzania anayechezea TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) Mmbwana Ally Samatta amenyakua tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika anachezea ndani ya bara la Afrika, wakati tuzo ya mwanasoka bora barani Afrika ikienda kwa Pierre-Emerick raia wa Gabon anayesakata kabumbumbu katika klabu ya Borussia Dortmund ya Ujerumani.
Tuzo hizo za kila mwaka zinazotolewa na Shirikisho la soka barani Afrika almaarufu kama CAF zimetolewa usiku kuamkia leo mjini Abuja nchini Nigeria.
Kwa upande wa timu ya wanawake ya mwaka tuzo imekwenda kwa timu ya Cameroon. Timu bora kwa wanaume kwa mwaka uliopita ni kutoka Ivory Coast.
Kocha bora wa mwaka ni – Herve Renard, kutoka Cote d’Ivore ambayo inashinda kwa mwaka wa pili mfululizo wakati Klabu bora ya soka barani Afrika ni – TP Mezembe, kutoka DR Congo ambapo mwanasoka bora wa kike Afrika ni Gaelle Enganamouit kutoka Cameroon na Mwamuzi bora wa mwaka ni – Bakary Gassama kutoka nchini Gambia.
Tuzo hizo zilipambwa na shamra shamra za kila aina kutoka kwa wasanii maarufu pamoja na wanenguaji walitumbuiza akiwemo mwanamuziki nguli kutoka nchini Mali, Salif Keita pamoja na mwanamuziki kutoka Nigeria Omowumi.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin