Aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe amepinga uamuzi wa kufutwa kwa matokeo yote ya uchaguzi visiwani Zanzibar
Amesema inashangaza kuona uchaguzi ulifutwa kwenye majimbo yote, badala ya yale yaliyokuwa na matatizo tu “Kilichotokea Zanzibar kimeihuzunisha dunia,” alisema mbunge huyo wa zamani wa Mtama mkoani Lindi. “Watanzania waelewe, kilichoishitua dunia ni kule kufuta matokeo kwa ujumla wake.
Yaani majimbo yote hakuna hata moja lililofanya vizuri? Hapa ndipo tunapata kigugumizi. Sasa tunakwenda wapi, tunafanya kitu gani? “Ilitakiwa kuwe na ubaguzi; majimbo mawili, matatu, manne, matano, haya hayajafanya vizuri ndiyo uchaguzi urudiwe. Kaubaguzi kale kangewekwa, hiyo ingefanana na sura ya dunia ya haki.