Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM na mbunge wa zamani wa Simanjiro Christopher Ole Sendeka amewataka watanzania kuwa makini na kuzipuuza kauli zinazoenezwa na baadhi ya watu kwenye mitandao kuwa serikali ya Dk John Magufuli imekuwa na baraza kubwa la mawaziri kuliko alivyo ahidi na kwamba serikali inaweza kuwa nagharama zaidi kwakuwa kauli hizo zinalengo la kufifisha juhudi za serikali ya awamu ya tano kufanya mabadiliko ya kiuchumi kwa watanzania.
Mwanasiasa huyo mkongwe aliyekuwa mjumbe wa kamati ya kampeni ya CCM katika uchaguzi mkuu uliopita amesema kimsingi Raisi Magufuli anatembea kwenye ahadi alizo zitoa za kuifanya Tanzania kuwa mpya na kikatiba makatibu wakuu na manaibu wao siyo wajumbe wa baraza la mawaziri kama inavyo potoshwa na baadhi ya watu.
Hivi karibuni,aliyekuwa Naibu Waziri wa Kazi na Ajira katika serikali ya awamu ya nne , Dk Makongoro Mahanga alisema uwingi wa makatibu wakuu unakinzana na dhana ya Rais Magufuli ya kupunguza ukubwa wa Baraza la Mawaziri.
Mahanga alimkosoa Rais Magufuli akisema ameongeza ukubwa wa Baraza la Mawaziri baada ya kuteua makatibu wakuu 27 wakati anawaaminisha wananchi kwamba wizara ni 15 tu.
Social Plugin