Barua ya notisi kutoka ofisi ya mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga iliyoandikwa tarehe 7 Januari mwaka 2016 ikiwataka wahusika wa bar hiyo wabomoe sehemu iliyoko katika eneo la hifadhi ya barabara ya Uhuru na ile ya kuelekea soko la Nguzo nane.Manispaa hiyo ilitoa siku 7 watekeleze agizo hilo,leo Januari 14,2016 siku ya 7 tangu agizo litolewe tinga tinga limefika eneo la tukio la kubomoa sehemu ya bar hiyo
Wakurugenzi wa Dragon Pub wameiambia Malunde1 blog kuwa walipata vibali vya kujenga bar hiyo kutoka serikalini lakini leo wanashangaa kuona tinga tinga likibomoa bar yao wakati walifuata utaratibu wote.
Wakazi wa Shinyanga wakiwa eneo la tukio wakishuhudia tukio hilo,ambapo wahusika wa bar hiyo wanasema wana leseni za biashara yao na kwamba walipewa ruhusa ya kujenga bara hiyo katika eneo hilo lakini wanashangaa kwa nini leo manispaa imegeuka
Tinga tinga likivunja Dragon Pub
Muonekano wa bar hiyo kwa ndani
Mmoja wa wakurugenzi wa Dragon Pub bwana Humphrey Geofrey akizungumza na waandishi wa habari ambapo alielezwa kusikitishwa na kitendo cha kubomolewa bara yao wakati walifuata utaratibu wote wa ujenzi huku akiitupia lawama halmashauri ya manispaa ya Shinyanga kwa kuendesha zoezi la ubomoaji kwa ubaguzi akidai kuwa bar na maduka mengi mjini Shinyanga yamejengwa karibu la barabara kwanini leo wameanza kubomoa Dragon Pub ambayo imeanza kufanya kazi hivi karibuni.Geofrey alisema ni vyema serikali ikatekeleza wajibu wake kwa kuzingatia usawa badala ya kuonea baadhi ya watu.
Wakurugenzi wa Dragon Pub wakizungumza na waandishi wa habari waliofika eneo la tukio.Wakurugenzi hao wa Dragon Pub mbali na kuitupia lawama manispaa ya Shinyanga kwa kubomoa ndani ya siku 7 walizokuwa wamepewa kubomoa kwa hiari yao,ambazo zilikuwa hazijaisha,wameiomba serikali kutenda haki kwa kila mwananchi badala ya wachache kuonekana wanafaa zaidi.Aidha wamesema zoezi hilo la ubomoaji mbali na baadhi ya mali zao kuharibiwa pia limewaathiri kibiashara pamoja na kuhatarisha ajira za wakazi wa Shinyanga ambao wamekimbilia katika bar hiyo ya kisasa kwa ajili ya kupata ajira
Muonekano wa Dragon Pub kwa nje baada ya baadhi ya sehemu za jengo hilo kubomolewa leo asubuhi
Wananchi wakishangaa kilichotokea huku wengine wakihoji kwanini serikali inafanya kazi kwa kunyanyasa baadhi ya watu,Dragon Pub imejengwa hivi karibuni lakini kuna bar na maduka mengi yapo karibu na barabara lakini hayavunjwi ina maana wao wako juu ya sheria??,walihoji wananchi hao
Kulia ni barabara ya kuelekea soko la Nguzo Nane ambayo pia ndiyo chanzo cha bar hiyo kubomolewa
Mmoja wa wafanya kazi wa Dragon Pub
Muonekano wa Dragon Pub baada ya baadhi ya sehemu za jengo hilo kubomolewa
Kulia ni barabara ya Uhuru ambayo pia ndiyo chanzo cha bar hiyo kubomolewa
Muonekano wa Dragon Pub baada ya kubomolewa
Dragon Pub baada ya kubomolewa
Baada ya zoezi la ubomoaji kuisha
Dragon Pub katika muonekano mwingine baada ya sehemu ya jengo hilo kubomolewa
Barabara ya kuelekea Soko la Nguzo Nane
Muonekano wa Dragon Pub siku chache kabla ya kubomolewa,baadhi ya wateja wake wakinywa vinywaji-Picha kutoka Maktaba ya Malunde1 blog
Siku chache kabla ya Dragon Pub kubomolewa,DJ Ray akiwa katika bar hiyo ya Kisasa zaidi mjini Shinyanga-Picha kutoka Maktaba ya Malunde1 blog
Tazama Video hapa chini wakati Tinga Tinga likibomoa Dragon Pub
Social Plugin