Picha 21!! WAANDISHI WA HABARI SHINYANGA WAIBUKIA KWENYE KIWANDA CHA MAFUTA CHA WACHINA,JIELONG HOLDINGS (T) LTD
Tuesday, January 26, 2016
Waandishi wa habari wakielekea katika
Kiwanda cha Mafuta ya kula ya Alizeti na Pamba cha Jielong
Holdings(T) LTD kilichopo katika eneo la Nhelegani manispaa ya Shinyanga katika ziara yao kujionea jinsi kinavyofanya shughuli zake na kusikiliza malalamiko mbalimbali kutoka kwa wafanyakazi wa kiwanda hicho.
Nje ya kiwanda cha Jielong
Holdings(T) LTD
Waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga wakiwa ndani ya kiwanda cha Jielong
Holdings(T) LTD,wa pili kutoka kushoto ni afisa utawala wa kiwanda hicho Joseph Francis Warioba akiwaongoza waandishi hao wa habari Afisa utawala wa kiwanda chaJielong
Holdings(T) LTD Joseph Francis Warioba akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari
Mwandishi wa habari wa Channel Ten John Mponeja akiuliza swali kwa mkurugenzi wa kiwanda cha Jielong
Holdings(T) LTD bwana Jerry Qi
Afisa utawala wa kiwanda cha Jielong
Holdings(T) LTD Joseph Warioba akiwaeleza waandishi wa habari kuhusu namna wanavyopakia mafuta baada ya uzalishaji huku akiongeza kuwa hivi sasa wamesimamisha uzalishaji wa mafuta ya pamba na alizeti kutokana na kukosa malighafi
Mafuta ya kupikia yakiwa tayari kupelekwa kwa walaji
Afisa utawala wa kiwanda cha Jielong
Holdings(T) LTD Joseph Warioba akionesha sabuni inayotengezwa katika kiwanda,hicho kwani mbali na kuzalisha mafuta ya kula,mabaki ya malighafi huyatumia kutengeneza sabuni maarufu kwa jina la Gwanji
Afisa utawala wa kiwanda cha Jielong
Holdings(T) LTD Joseph Warioba akionesha gwanji
Shughuli ya kutengeneza ndoo inaendelea kiwandani hapo
Wanatengeneza ndoo.....
Tunatengeneza ndoo na kuweka lebo kwenye ndoo.....
Viongozi wa kiwanda cha Jielong
Holdings(T) LTD Joseph Warioba wakionesha mafuta ya kupikia kwa waandishi wa habari
Mkurugenzi wa kiwanda cha Jielong
Holdings(T) LTD Joseph Warioba akiwaeleza jambo waandishi wa habari,Marco Maduhu na Kadama Malunde(kulia)
Waandishi wa habari wakiwa ndani ya kiwanda cha Jielong
Holdings(T) LTD wakiwa na viongozi wa kiwanda hicho
Afisa utawala wa kiwanda cha Jielong
Holdings(T) LTD Joseph Warioba akizungumza na waandishi wa habari
Mkurugenzi wa kiwanda cha Jielong
Holdings (T) LTD Jerry Qi akizungumza na waandishi wa habari
Waandishi wa habari wakizungumza na viongozi wa kiwanda cha Jielong
Holdings(T) LTD Joseph Warioba
Kulia ni afisa mahusiano wa kiwanda cha Jielong
Holdings(T) LTD Lilian Sisawa,kushoto ni mwandishi wa habari Chibura Makorongo
Waandishi wa habari wakizungumza na viongozi wa wa kiwanda hicho Jengo la utawala la kiwanda cha Jielong
Holdings(T) LTD Kiwanda cha Mafuta ya kula ya Alizeti na Pamba cha Jielong Holdings(T) LTD kilichopo katika manispaa ya Shinyanga kinakabiliwa na ukosefu malighafi hali inayosababisha kisifanye uzalishaji na kuleta changamoto ya ajira kwa wakazi wa Shinyanga.
Akizungumza mwishoni mwa wiki iliyopita baada ya waandishi wa habari kufanya ziara katika kiwanda hicho mkurugenzi wa kiwanda hicho Jerry Qi alisema kutokana na uhaba wa malighafi za kuzalishia mafuta hayo wanalazimika kuzima mitambo yao.
Qi alisema hivi sasa zoezi la kutengeneza mafuta linasuasua kutokana na kukosa malighafi hizo huku akitoa wito kwa wakulima nchini kupeleka alizeti na pamba yao katika kiwanda hicho.
Katika hatua nyingine Qi alitaja changamoto nyingine wanayokabiliana nayo kuwa ni pamoja na mtazamo hasi kwa wananchi juu ya kiwanda hicho kwani kuna uzushi unaoenezwa kuwa hawatoi mikataba kwa wafanya kazi wao.
Kwa upande wake afisa Utawala wa Kiwanda hicho Joseph Warioba alikanusha madai ya baadhi ya wafanya kazi wa kiwanda hicho wakiwemo madereva kuwa wamekuwa wakinyanyaswa na viongozi wa kiwanda hicho ikiwemo kufanyishwa kazi zaidi ya wa muda wa kazi na mikataba yao.
Warioba alisema kiwanda hicho kimekuwa kikitoa mikataba kwa kuzingatia sheria za nchi na kwa upande wa madereva wa magari wamekuwa wakiwakata mishahara yao hasa pale wanapokiuka sheria za barabarani na kutozwa faini mfano wanapoendesha magari kwa mwendo kasi.
“Kinachotusumbua hapa ni wafanya kazi kutokuwa na elimu ya kutosha,mambo mengi hawaelewi,kuna wengine ukiwakata pesa za mifuko ya kijamii mfano NSSF,wanagoma kufanya kazi wakati kiutaratibu wanapaswa kujiunga na mifuko hiyo,wengine hawafiki kabisa kazini tena bila taarifa lakini anataka alipwe”,alieleza Warioba.
Hata hivyo wafanya kazi wa kiwanda hicho waliozungumza na gazeti hili waliogoma kutaja majina yao wakiogopa kuhatarisha ajira zao walisema wamekuwa wakinyanyaswa ikiwemo kupigwa,kukatwa mishahara yao bila sababu zinazoeleweka,ikiwemo kuchelewa kazini ingawa kiwanda hakina magari kwa ajili ya kuwasafirisha na huwa wanatumia gharama zao kusafiri.
Walisema madai mengine ni kutolipwa pesa za likizo,kutotibiwa wanapougua,kutopewa ruhusa hata kama umefiwa,madereva kukatwa sehemu ya mishahara yao hasa pale gari linapoharibika ikiwemo matairi kuisha,pesa kidogo wakati wa safari ndefu,mishahara midogo wanayolazimika kugawana na makondakta wao.
Na Kadama Malunde-Malunde1 blog Shinyanga
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin