RAIS MAGUFULI ATAFUKUZA KAZI MKUU WA MKOA KAMA ATASIKIA WANANCHI WANALIA NJAA
Friday, January 22, 2016
Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh John Magufuli amesema kuanzia sasa hataki kusikia malalamiko ya wananchi juu ya suala la njaa na ikitokea akasikia vilio hivyo vikiendelea mkuu wa mkoa husika atachukuliwa hatua ikiwemo ya kufukuzwa kazi.
Mh. Magufuli ambaye yuko katika ziara ya kikazi mkoani Arusha ameyasema hayo alipokuwa njiani kutoka jijini Arusha kwenda wilaya Monduli kwa ajili ya kufunga mazoezi ya kijeshi ya kuonyesha uwezo wa medani 2016 yaliyofanyika katika Briged ya 303 iliyoko Monduli.
Aidha Mh rais Dr. Magufuli amesema ni jambo halikubali kuendelea kusikia malalamiko ya wananchi juu ya mambo yaliyoko ndani ya uwezo na yanayoweza kutatuliwa na wakuu wa mikoa na ameendelea kuwataka viongozi na watendaji wa serikaali kutimiza wajibu ukiwemo wa kuwatumikia wananchi.
Kuhusu malalamiko ya wananchi juu ya kero ya rushwa mh Rais amewataka wananchi hao kuwa wapole kwani kero itashughulikiwa na itapata ufumbuzi kwani zoezi la kutumbua majipu linaendelea na kwamba kinachofanyika sasa ni kutumbua majipu yaliyoiva ambayo ni sehemu ndogo tu ya majipu yaliyopo.
Mh Rais kesho anatarajiwa kutoa kamisheni kwa askari wanafunzi katika chuo cha mafunzo ya kijeshi cha TMA monduli.
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin