Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

RAIS MSAAFU JAKAYA KIKWETE ATINGA IKULU KWA MAGUFULI,WAFANYA MAZUNGUMZO,AMFAGILIA KWA KASI YAKE




Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amekutana na kufanya mazungumzo na Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete Ikulu Jijini Dar es salaam.

Katika Mazungumzo hayo Rais Mstaafu Kikwete amemtakia Rais Magufuli heri ya Mwaka mpya na kumpongeza kwa uongozi mzuri.

Rais Kikwete pia amesema anaunga mkono juhudi mbalimbali zinazofanywa na Rais Magufuli ikiwemo ukusanyaji wa mapato ya serikali.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizungumza na Rais Mstaafu wa Awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Ikulu jijini Dar es Salaam

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akifurahia jambo na Rais Mstaafu wa Awamu ya nne, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete mara baada ya kumaliza mazungumzo Ikulu Jijini Dar es Salaam.

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com