RAIS MSTAAFU JAKAYA KIKWETE ATUNUKIWA SHAHADA YA HESHIMA YA UDAKTARI WA FALSAFA YA MAHUSIANO YA KIMATAIFA





Rais mstaafu wa awamu ya nne Mhe Dkt Jakaya Mrisho Kikwete ametunukiwa Shahada ya heshima ya udaktari wa falsafa ya mahusiano ya kimataifa jana Jijini Dar es Salaam katika mahafaliya 30 ya Chuo Kikuu Huria Tanzania.


Mhe. Dkt Jakaya Mrisho Kikwete amesema amefarijika sana kutunukiwa Shahada hiyo ya heshima itolewayo na Chuo kikuu Huria Tanzania kwa watu ambao wametoa mchango katika maendeleo katika jamii kupitia nafasi zao kiutendaji.



“Naipokea heshima hii toka Chuo Kikuu Huria Tanzania kwa moyo mmoja kwani wameona mchango ambao nimeutoa nilipokuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa Awamu ya Nne hivyo basi nitaendeleza mahusiano na ushirikiano kimataifa”.Alisema Mhe. Dkt Kikwete.


Mbali na Dkt Jakaya Mrisho Kikwete kuna baadhi ya maraisi na wakuu mbalimbali duniani waliwahi kupata Shahada za heshima toka Chuo Kikuu Huria Tanzania ambao ni Rais wa Awamu ya Kwanza wa Tanzania Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Rais wa Awamu ya Pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi, Rais wa Awamu ya Tatu Benjamin William Mkapa, Rais wa zamani wa Afrika ya Kusini Hayati Nelson Mandela na Dkt Koichiro Mastuura Mkurugenz iwa UNESCO.


Chuo kikuu Huria cha Tanzania kimetoa jumla ya wahitimu 69 wawili Shahada maalum na 67 ni Shahada, Stahahada na Astashahada, ambapo Shahada ya uzamivu ni wahitimu watatu, Shahada ya uzamili ni wahitimu 20, Shahada wahitimu 22,Stashahada wahitimu 15 na Astashahada wahitimu 6.


Tangu kuanzishwa kwa Chuo Kikuu Huria Tanzania mwaka 1992 jumla ya wahitimu 25,908 wametunukiwa Shahada mbalimbali na haya ni mahafali ya 30 tangu chuo kuanzishwa



Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania Dkt Asha Rose Migiro akimpongeza Rais mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe Dkt Jakaya Mrisho Kikwete baada ya kumtunuku Shahada ya heshima ya udaktari wa falsafa ya mahusiano ya kimataifa katika maafali ya 30 ya Chuo kikuu Huria Tanzania yaliyofanyika jana Jijini Dar es Salaam.



Rais mstaafu wa Awamu ya Nne Mhe Dkt Jakaya Mrisho Kikwete akiongea na wanataaluma na wageni katika maafali ya 30 ya Chuo kikuu Huria Tanzania yaliyofanyika jana Jijini Dar es Salaam



Mkuu wa Chuo Kikuu Huria Tanzania Dkt Asha Rose Migiro akifungua rasmi mahafali ya 30 ya Chuo Kikuu Huria Tanzania yaliyofanyika jana Jijini Dar es Salaam

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post