Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

SERIKALI IMETUMIA SHILINGI BIL 459 KUKOPESHA WANAFUNZI WA ELIMU YA JUU MWAKA 2015/2016

 
Serikali imetumia bilioni 459 kuwakopesha wanafunzi wa elimu ya juu katika kipindi cha mwaka 2015/2016 ambapo jumla ya wanafunzi 122,486 wamenufaika.


Hayo yamesemwa na Meneja wa Habari Elimu na Mawasiliano wa Bodi ya Mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya Juu Bw. Omega Ngole wakati wa mkutano na waandishi wa Habari leo Jijini Dar es salaam.


“Walionufaika na mikopo katika kipindi cha 2015/2016 ni wengi na haijawahi kutokea katika Historia tangu kuanzishwa kwa Bodi na haya ni matokeo ya utendaji mzuri wa Serikali ya awamu ya tano “alisisitiza Ngole

Akizungumzia utolewaji wa mikopo Katika kipindi cha mwaka 2014/2015 Ngole alibainisha kuwa jumla ya wanafunzi 99,069 walipata mikopo na jumla bilioni 341 zilitolewa .


Pia Ngole alibainisha kuwa Serikali imeongeza idadi ya wanaufaika wa mikopo kwa kuzingatia vipaumbele vinavyotokana na mahitaji ya Taifa.


Ngole amebainisha kuwa mafanikio hayo ni matokeo ya utekelezaji wa Falsafa ya Serikali ya awamu ya tano inayosema Hapa Kazi tu.


Aliongeza kuwa Bodi hiyo inaendelea kufanya kazi kwa kuzingatia kasi ya Serikali ya awamu ya tano itakayowezesha kutoa mikopo kwa wakati kwa kuzingatia sheria Kanuni. na Taratibu za utoaji mikopo.


Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya juu ni Taasisi ya Serikali iliyoanzishwa kwa mujibu wa sheria Na.9 ya mwaka 2004 na kuanza rasmi mwezi julai, 2005 ambapo Katika mwaka wa Masomo 2005/2006 idadi ya wanafunzi waliopata mikopo ilikuwa 42,749 ambapo jumla ya bilioni 56.1 zilitolewa

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com