Rais Jimmy
Wako mastaa waliojaribu maisha kwenye upande mwingine Tanzania, wako waliotoka kwenye game ya muziki na wengine walitoka kwenye movie… kwa maamuzi ya dhati kabisa wakajitangaza kwamba wanaitaka siasa !!
Wapo waliotoboa, wakafanikiwa kupata nafasi walizogombea kwenye Ubunge na Udiwani lakini wako ambao mambo hayakwenda sawa na wakaahidi kwamba wanaingia mtaani kujipanga rasmi kwa ajili ya jukwaa la kampeni za 2020 Tanzania.
Kama ambavyo mwigizaji Schwarzenegger aliwahi kuwa Gavana wa Jimbo la California kuanzia mwaka 2003 mpaka 2011… hiyo ni nafasi kubwa sana kwa Marekani, lakini mwingine kutoka kwenye mikono ya sanaa ya uigizaji na vichekesho Guatemala, Jimmy Morales ameshinda kiti cha Urais na tayari kaapishwa.
Rais huyo mpya hana uzoefu na masuala ya siasa ila ahadi yake ya kwanza ni kupambana na rushwa…
Hizi hapa video ya Jimmy Morales akiwa anaapishwa nchini kwao Guatemala na nyingine katika moja ya video zake akichekesha
Social Plugin