Hali ya sintofahamu imeendelea ndani ya bunge baada ya wabunge wote wa Upinzani kutoka ndani ya bunge mara baada ya Wabunge kuanza kuchangia hotuba ya Rais.
Baada ya kipindi cha Maswali na Majibu, yalifuata matangazo na baada ya Matangazo, wabunge wakaanza kuchangia hotuba ya Rais Magufuli .
Wakati hayo yakiendelea, wabunge kadhaa wa UKAWA akiwemo mbunge wa Ubungo(chadema), Saed Kubeneawalikuwa wakiomba muongozo wa Naibu Spika ili waongee lakini hawakupewa nafasi.
Naibu Spika alikataa miongozo hiyo na kulitaka Bunge lijikite katika kujadili Hotuba ya Rais. Hali hiyo iliwakera wabunge wa upinzani kwa madai kuwa wamezibwa midomo na hivyo wakaamua kutoka nje ya ukumbi wa bunge
Social Plugin