Jeshi la Polisi kanda maalum ya Dar es Salaam, limefanikiwa kuwanasa wafanyabiashara wakongwe wa dawa za kulevya nchini ambao pia wanadaiwa kufanya biashara haramu za binadamu ambao wamekuwa wakiwasafirisha kutoka nchini kwenda katika nchi zinazozalisha dawa za kulevya.
Magwiji hao wa dawa za kulevya nchini waliotiwa nguvuni na jeshi la polisi ni pamoja na Mohamed Abdallah Omary, Nassoro Suleiman na meneja wa duka la Tungwe Bureau de Change ambalo hutumika kusafirisha fedha za dawa za kulevya kwenda nchini Pakstani kinyume na sheria.
Taarifa hiyo kamanda Sirro, amesema kwasasa jeshi la polisi limejipanga kuhakikisha linadhibiti mianya yote ya dawa za kulevya ambapo pia katika msako mkali uliofanyika mwishoni mwa wiki gari zenye namba za usajili T271 DCT, T916 DCL, T593 CEL na T999 DDB zimekamatwa.
Kamanda Sirro amesema kuwa kumeibuka wimbi la wafanyabiashara wa dawa za kulevya kusafirisha watanzania kuwapeleka nchini Pakstani na kuwaacha kama bondi ili wapatiwe mzigo mkubwa wa dawa za kulevya ambapo wengi wao wamekuwa wakiuawa ambapo amesema jeshi limejipanga kusambaratisha mtandao huo.
Via>>ITV
Social Plugin