Wananchi wa kata ya Kambarage wakiaga mwili wa Emilian Kulwa anayedaiwa kufariki katika mazingira ya kutatanisha-Picha zote na Marco Maduhu-Malunde1 blog
Awali wananchi wakiwa katika eneo la tukio wakimsikiliza diwani wa kata hiyo Hassan Mwendapole
Diwani wa kata ya Kambarage Hassan Mwendapole akiwasihi wananchi wasifanye vurugu msibani
Mwili wa marehemu ukiletwa kutoka hospitalini
Katika
hali isiyo ya kawaida wananchi wa mtaa na kata ya Kambarage Manispaa ya
Shinyanga wamezua kizaazaa msibani wakishinikiza kuaga mwili wa marehemu
Emiliani Kulwa (26) aliyefariki dunia katika mazingira ya kutatanisha baada ya
kuanza kupandisha majini na kutamka maneno yasiyoeleweka.
Taharuki
hiyo ilitokea jana jioni baada ya mwili wa marehemu kushindwa kuwasilishwa
msibani kwa ajili ya wananchi kuuaga kwa madai kuwa umeharibika vibaya na
hauwezi kuagwa.
Mwili
wa marehemu ulitakiwa uwasilishwe msibani hapo majira ya saa kumi jioni kwa
ajiri ya wananzengo kuuaga na kisha urudishwe mochwari kuandaliwa kwa safari ya
kupelekwa kwao na marehemu Moshi mkoani Kilimanjaro kwa ajili ya mazishi.
Wakati
wananchi hao wakisubiri mwili wa marehemu kuletwa kutoka hospitali ya rufaa ya
mkoa wa Shinyanga ghafla wanazengo ambao walitumwa kuufuata walirudi huku gari
likiwa tupu, wakati jamii ikitangaziwa ikaupokee lakini cha ajabu wakakuta
mwili huo haupo ndipo vurugu, miruzi, yowe zilipoanza kutawala msibani hapo.
Baada
ya hali kuendelea kuwa mbaya diwani wa kata ya Kambarage Hassan Mwendapole
alifika eneo la tukio na kutuliza hasira za wananzego na na hatimaye mwili ukaletwa msibani hapo majira
ya saa 12 jioni hali iliyofanya wanazengo kuushangilia na hatimaye vurugu
kuisha.
Mdau wa Malunde1 blog Agnes Lema kutoka Kambarage aliyekuwa eneo la tukio ameisimulia blog hii kuhusu tukio
hili….
“Kuna huyo
kijana aliugua kichwa akapelekwa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga inadaiwa
kuwa hakuwa na damu ..akiwa hospitalini
akaongezewa ..kisha kuna maombi yalifanyika mara akapandisha majini,jini likawa
linasema limetumwa ila halijataja limetumwa na nani….
Ikabidi
kijana atolewe hospitali arudishwe nyumbani…basi
ikawa mara maombi mara waganga wa kienyeji sasa akiwa home kwao hapa jirani, ndiyo
mauzauza yakawepo sasa hasa nyakati za usiku….
Mara
mgonjwa awataje watu wanaojulikana hapa hapa mtaani kwamba “Niacheni
mnanichukua mie wanini sasa wakati sina hata kitu..Basi mambo mengi yakawa
yanatokeo ndani ,wakifanya maomba jini linapanda likaongea mengi sikuwepo ila
kwa maelezo kuwa ni lazima afe..
Kutokana
na mauza uza hayo ikabidi ndugu waite ambaye naye aliomba dua akasema “Huyu
Jini mkubwa mpaka aje Mtu mwenye Jini mkubwa zaidi ya huyu”,Anasimulia Agnes Lema.
“Asubuhi
yake ndiyo mgonjwa alifariki dunia kwani alikuwa hoi hainuki wala nini ..pia
kuna taarifa kuwa usiku huo aliinuka na kufungua mlango kisha kutoka nje mpaka
kwenye chumba ambacho hakijaisha kujengwa akawa anaita majina flani na
kuwaambia “Mnanipeleka wapi basi kateni fensi ili nipite mbona sioni ninapoenda…
na mnaning’ang’ania nimewakosea nini”….
Mambo
mengi alizungumza , kakaake akamwambia kama wamegoma kukata fensi turudi,
akarudi kitandani akakaa na kuongea na ndugu yake mambo mengi pia, asubuhi
kulipokucha akawaambia nduguze muda umefika mie naenda maana nimewaomba mno
waniache wamegoma mie naenda sasa, akakoroma na kufariki dunia.
…Sasa
kilicholeta shida ni mwenyekiti wa mtaa akalazimisha ndugu kuwa mwili uletwe nyumbani
uagwe then urudishwe mochwari halafu ndiyo
mwili usafirishwe kwenda kwao Moshi…basi ndugu wakawa hawataki mwili uletwe
nyumbani siku bali siku inayofuata….”,anasimulia Agnes Lema.
“Emilian
amekufa katika mazingira ya utata ugonjwa wake haujulikani,tunaambiwa amefariki
kwa kuumwa kichwa na shingo, na kipindi anaumwa tulipokuwa tunakuja kumsalimia
hapa nyumbani kwake, ndugu zake walituzuia hakuna mtu yeyote kumuona, ndipo
tarehe 19 mwezi huu tukasikia amefariki, halafu sasa hivi tusimuage
tulipewa taarifa ya nini” ,anaeleza shuhuda mwingine aliyejulikana kwa
jina la Nyorobi.
Kufuatia
tukio hilo Mwenyekiti wa mtaa huo wa mtaa huo Fatuma Juma aliutangazia umma
kuwa familia ya marehemu imepigwa faini ya shilingi 500,000/= kwa kucheza na
akili za wanazengo.
Inaelezwa
kuwa Emilian amefariki kwa kuumwa kichwa na shingo na kwamba ameacha mjane na
mtoto mmoja Neema Kulwa(01), na tayari Mwili wake umesafirishwa leo kwenda
Moshi kwa ajili ya mazishi.
Hata hivyo taarifa zilizoifikia Malunde1
blog ni kwamba ndani ya familia ya marehemu kuna mmoja anatuhumiwa kuwa ni
mchawi na jamii imejawa na imani za
kishirikina kuwa huenda ndiyo amemtoa kafara kijana huyo ambaye ni mtoto wa
dadake.
Malunde1 blog bado inafuatilia kwa undani
kuhusu tukio hili..tutawaletea habari zozote tutakazozipata..
Manispaa ya Shinyanga ni miongoni mwa
maeneo ambayo baadhi ya watu wake wanaimani za kishirikina, ni hivi karibuni tu
watu wawili walifariki dunia katika mazingira ya kutatanisha kwa kile
kilichodaiwa kuwa walifariki kwa shoti ya umeme kwenye nyumba isiyo na umeme
vifo ambavyo mpaka sasa chanzo chake hakijulikani.
Na Marco Maduhu na Malunde1
blog Shinyanga.