Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

BASI LA NATA RAHA LAUA WATU SABA NA KUJERUHI ZAIDI YA 50 HUKO BUNDA BAADA YA KUPARAMIA NYUMBA YA MTU



Watu saba wamefariki wamefariki dunia na wengine zaidi ya 56 kujeruhiwa vibaya baada ya basi la abiria la Nata Raha yenye namba za usajili T 473 CJN linalofanya safari zake kati ya Mugumu wilayani serengeti kupitia Bunda kwenda mkoani Mara kupalamia nyumba eneo la njia nne mjini Bunda baada ya breki za basi hilo kukatika likiwa katika mteremko mkali. 
 
 
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya ya Bunda Bw Joshua Mirumbe, ambaye pia ni mkuu wa wilaya ya Bunda, akizungumza baada ya kufika eneo la tukio, amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo majira ya saa tano asubuhi na kusema kati ya majeruhi hao wanane wamepelekwa hospitali ya rufaa ya Bugando jijini Mwanza huku wengine wakilazwa hospitali teule ya DDH mjini Bunda. 
 
 

Baadhi ya majeruhi wa ajali hiyo wamedai baada ya kukaribia njia kuu ya Mwanza Musoma mita chache tu kufika kituo kikuu cha mabasi mjini Bunda mwendo wa basi hilo uliongezeka na baada ya kuhoji walielezwa kuhusu kukatika kwa breki hizo kabla ya kuvamia jengo hilo. 
 

Hata hivyo wakati mwenyekiti huyo wa kamati ya ulinzi na usalama akisema walifariki ni abiria saba lakini kamanda wa polisi mkoa wa Mara ACP Philip Alex Kalangi akizungumza na ITV kwa njia ya simu amesema abiria sita ndiyo waliofariki katika ajali hiyo.
 

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com