Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

BASI LA MASHIMBA EXPRESS LA KAHAMA- MWANZA LAGONGANA NA GARI NDOGO NA KUUA WATU WANNE


Kondakta wa basi la Mashimba Exress akiwa eneo la tukio

Basi la Mashimba Expess likiwa limeharibika
Mashimba Express


Gari ndogo
Watu wane wamefariki dunia katika ajali iliyohusisha basi la Mashimba Express lililokuwa linasafiri kutoka Kahama kwenda jijini Mwanza kugongana na gari dogo  katika eneo la kijiji cha Bubiki kata ya Songwa wilayani Kishapu katika barabara ya Shinyanga kuelekea Mwanza

Ajali hiyo imetokea leo jioni ambapo mashuhuda wa tukio hilo wameiambia Malunde1 blog kuwa gari ndogo ilikuwa katika mwendo kasi na watu wawili kutoka katika gari hilo akiwemo dereva wamefariki dunia. 

Malunde1 blog imefika katika hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga na kushuhudia baadhi ya majeruhi wakipatiwa matibabu. 

Mganga mfawidhi wa hospitali hiyo Dkt Albert George Masigati amesema kati ya saa 12 na saa moja usiku huu wamepokea miili ya marehemu wanne katika hospitali hiyo  na majeruhi wanane.  

Dkt Masigati amesema hakuna majeruhi aliye katika hali mbaya na kwamba bado wanaendelea kuwafanyia uchunguzi kutokana na kwamba wamepata michubuko mbalimbali katika miili yao. 

Mmoja wa abiria katika basi hilo aliyejitambulisha kwa jina la Ramadhan aliyelazwa katika hospitali ya rufaaa ya mkoa wa Shinyanga amesema basi lao lilikuwa katika mwendo wa kawaida lakini gari dogo ndiyo lilikuwa katika mwendo kasi. 

 SOMA HABARI KAMILI HAPA
Na Kadama Malunde-Malunde1 blog

BOFYA HAPA KUONA PICHA NYINGI ZAIDI

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com