SIMBA YAONESHA UBABE KWA STAND UNITED,MATOKEO YA MECHI ZINGINE ZOTE LEO YAKO HAPA
Saturday, February 13, 2016
Licha ya kuwa Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania bara klabu ya Dar Es Salam Young African wapo Mauritius kukipiga na klabu ya Cercle De Joachim katika harakati zake za kuanza kuwania taji la klabu Bingwa Afrika, Ligi Kuu Tanzania bara imeendelea leo February 13 kama kawaida kwa michezo mitano kupigwa katika viwanja tofauti.
Simba walikuwa Shinyanga kumenyana na wenyeji wao Stand United chama la wana, katika mchezo wao wa 19 wa Ligi Kuu, Simba ambayo iliingia ikiwa na kumbukumbu ya kutoka na ushindi wa goli 1-0 mchezo wake wa mwisho katika uwanja huo dhidi ya Kagera Sugar, ilifanikiwa kuendeleza rekodi ya ushindi.
Simba imefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 2-1, shukrani kwa Simba ziende kwa Hamis Kiiza Diego, aliyefanikiwa kupachika goli zote mbili dakika ya 37 na 47, huku kwa upande wa Stand United goli la kufutia machozi lilifungwa na Pastore Atanus dakika ya 89, baada ya kutumia vyema makosa ya mabeki wa Simba.
Kwa matokeo hayo Simba imetimiza jumla ya point 45 na kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi , ikiwa na jumla ya michezo 19. wakati Stand United wameendelea kusalia na point zao 29 na nafasi yao ya 5.
Matokeo ya mechi nyingine za Ligi Kuu zilizochezwa February 13 Mgambo JKT 0 – 1 African Sports Mbeya City 5 – 1 Toto Africans Ndanda FC 1 – 0 Majimaji JKT Ruvu 1-1 Kagera Sugar
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin