Malunde1 blog imepita katika ukurasa wa Facebook wa aliyekuwa naibu meya wa manispaa ya Shinyanga ndugu David Mathew Nkulila,ambaye sasa ni diwani wa kata ya Ndembezi katika manispaa hiyo kwa tiketi ya CCM,anayetajwa kuwa miongoni mwa madiwani wa CCM wenye msimamo mkali akidaiwa kuharibu ulaji wa baadhi ya watendaji katika serikali...ameandika ujumbe huu hapa chini na kupost picha ya mbwa....
"HILI NALO NI JIPU BAYA.
Kuna mazoea yaliojengeka nchini hapa ambayo mh Rais anaendelea na zoezi la kuyaondoa kwa kuyaita majipu.Tazama mbwa hao si mizoga! wako hai na mbele yake ni ofisi ya mtendaji wa kata ya Ndembezi manispaa ya shinyanga. Taarifa ilishafika manispaa ya kumba wauwawe ili kunusuru maisha ya watu na hasa watoto. Hawana chanjo na taarifa iliipo dawa za kichaa cha mbwa endapo patatokea mlipuko hakuna. Viongozi wapo hawashituki mpaka aje waziri atoe AGIZO. Agizo la Madiwani hayana uzito maana wameshasema!! au pengine mpaka aseme RC au DC? Hii Tanzania itakuwa ya viongozi wanaosubiri maagizo tu? Hiyo hawaioni ni hatari sawa na kipindupindu, malaria ambayo kinga zinahitajika? Sheria za ufugaji mbwa zimefutwa?? Waziri mkuu lione hili nalo ni jipu, Mbwa wanaozurula ni hatari saana na Hatari zaidi mlipuko ukitokea Dawa ni mashaka na matokeo ni vifo vya kusababishwa na watendaji/viongozi wazembe. Wadau mnasemaje? mimi nimesema saana mwisho napasua jipu kupitia FB"