Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

JAMAA AUAWA KATIKA CHUO CHA SAUTI MWANZA ALIPOKWENDA KUMTEMBELEA MPENZI WAKE HOSTEL,AKAONA SMS ZA MCHEPUKO,DADA AKAPIGA KELELE Mwiziiiiiii!!!




Kwa masikitiko makubwa tukio tajwa hapo chini limetokea Chuo cha SAUT Mwanza ambapo Jamaa wa jinsia ya kiume ,alienda kumtembelea mpenzi wake chuoni SAUT bweni la RUGAMBWA.



 Mmoja wa mashuhuda wa tukio hilo anasimulia kisa kizima:


Ukweli ni kwamba huyo jamaa na huyo dada ni wapenzi wa muda mrefu na pia jamaa sio mwanafunzi ni raia wa kawaida anayehusika na mambo hasa ya modeling na amekuwa akiandaa event mbalimbali kama mtakuwa na kumbukumbu vizuri kuna kipindi kulitokea shindano la MISS ALBINISM lililofanyika Mwanza huyu jamaa alikuwa miongoni mwa wahusika wa hilo shindano,na siku tatu zilizopita huyu jamaa alitoka kumzika baba yake mzazi.

Kilichotokea hapo ni baada ya jamaa kwenda hosteli za wanawake ambazo zipo ndani ya chuo ambapo ndipo alipokuwa akiishi huyo mpenzi wake, katika kukagua simu ndipo akakuta sms za utata, ukatokea ugomvi katika mabishano huyo dada akasema atamwita mwizi kama utani kweli akaita mwizi Mwizi!!

Jamaa kwa kuogopa na sababu hakuwa na kitambulisho ndipo akatoka mbio, hapo ndipo alipoharibu wananzengo na wanachuo bila kujali wakaanza kupiga na mpaka wanafika polisi alikuwa kapigwa sana, alipelekwa kituoni kutoa maelezo.


Baada ya hapo ndipo tukapata taarifa kafariki na hiyo ni sababu ya kipigo.

 Via>>Udakuspecially.com

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com