Kijana huyu anaitwa "Simon Shilage" ana umri wa miaka 22, Yeye kwa kushirikiana na mwenzie mmoja ambaye bado hajapatikana ndio waliomuua Diwani wa kata ya Kimwai huko Muleba Ndg.Faustine Muliga wa chama cha wananchi CUF.
Kijana huyu amekamatwa jioni ya jana na wananchi wa kijiji cha Kyota akijaribu kutoroka. Amekutwa na panga lenye damu alilotumia kumuua diwani Muliga. Alipohojiwa amekiri kwamba ni kweli yeye na mwenzie mmoja (hakumtaja jina) ndio waliomuua Mhe.Muliga kwa kumkata mapanga.
Amesema kazi hiyo walitumwa na aliyekua mgombea udiwani wa Kata hiyo kwa ticket ya CCM kwenye uchaguzi uliopita, ambaye alikua mpinzani wa Muliga lakini alishindwa kwenye uchaguzi. Ameongeza kuwa Mgombea huyo aliwaahidi kiasi cha shilingi milioni 1.5 ikiwa watafanikiwa kumuua Muliga na aliwapa "advance" ya shilingi laki moja na nusu (150,000/=). Baada ya makubaliano hayo vijana hao walimvamia Muliga nyumbani kwake majira ya saa 2 usiku akiangalia "Taarifa ya Habari" ambapo walimkata mapanga maeneo mbalimbali mwilini mwake kabla ya kutokomea kusikojulikana.
Kijana huyu alikamatwa na wananchi wenye hasira kali ambao walitaka kumuua lakini akaokolewa na Polisi. Hata hivyo wananchi hao walifanikiwa kumkata sikio lake moja la kushoto kama anavyoonekana pichani.
Kwa sasa anashikiliwa kituo cha Polisi Muleba kwa upelelezi, kabla ya kupandishwa Mahakamani kujibu tuhuma za Mauaji.!
Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa
Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Social Plugin