KESI YA MCHEZAJI WA SIMBA YA KUMSHAMBULIA MWANDISHI WA HABARI YAANZA KUSIKILIZWA SHINYANGA


Kesi inayomkabili mchezaji mkongwe wa timu ya Simba Mwinyi Kazimoto ya shambulizi la kudhuru mwili dhidi ya mwandishi wa habari wa kampuni ya Mwananchi Communications Ltd, Mwanahimba Richard imeanza kusikilizwa jana katika mahakama ya hakimu mfawidhi mkoa wa Shinyanga.


Akisomewa shtaka hilo mahakamani hapo na mwanasheria wa serikali Upendo Shemkole alisema mshtakiwa alitenda kosa la shambulizi la kudhuru mwili Februari 10,2016, katika uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga baada ya mazoezi alionekana kumshambulia mwandishi wa habari Mwanahimba Richard.


Hata hivyo mshitakiwa Mwinyi Kazimoto baada ya kusomewa shitaka hilo alikana kutenda kosa hilo , na kuiomba mahakama kumpatia mwezi mmoja ili atafute wakili wa utetezi wake ombi ambalo lilikubaliwa.

Hakimu mkazi , mfawidhi wa mahakama hiyo Rahim Mushi anayesikiliza kesi hiyo alisema kesi imeahirishwa hadi Machi 21 mwaka, huu ndipo itaendelea tena kusikilizwa ili kutoa fursa kwa mshitakiwa kupeleka wakili wake wa utetezi.

Jumla ya mashahidi sita wanatarajiwa kutoa ushahidi mahakamani hapo katika kesi hiyo inayomkabili kiungo mchezaji wa Simba Mwinyi Kazimoto, ambapo pia alipewa dhamana ya shilingi 500,000/= na mwanasheria wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga Batromeo Lwela.
Na Kadama Malunde- Malunde1 blog Shinyanga

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post