Kimenuka Shinyanga !! MADIWANI WALIANZISHA...KIKAO CHA BARAZA CHAVUNJIKA,CHANZO NI MKURUGENZI ANGALIA PICHA



Hapa ni ndani ya ukumbi wa mikutano wa halmashauri ya wilaya ya Shinyanga mjini Shinyanga ambako leo Jumanne Februari 23,2016 kulitakiwa kufanyike Kikao cha Baraza la Madiwani la madiwani wa manispaa ya Shinyanga,lakini kikao hicho kilivunjika ghafla baada ya madiwani kutoa hoja ya kutofanyika kwa kikao cha kujadili na kupitisha bajeti ya mwaka 2016/2017 kwa kile walichodai mkurugenzi wa manispaa hiyo Lewis Kalinjuna amekiuka kanuni za kuendesha kikao,pichani wajumbe wa kikao hicho wakitoka ukumbini baada ya naibu meya wa manispaa hiyo Agnes Machiya kuahirisha kikao hicho.


Wakichangia hoja ya kuahirishwa kwa kikao hicho  madiwani hao walisema kikao hicho ni batili na hakitakiwi kufanyika kutokana na kuitishwa kabla ya siku ya moja ya kufanyika kwa kikao hicho Februari 23,2016.
 
Madiwani hao kwa pamoa wamedai kuwa mkurugenzi wa manispaa hiyo amevunja kanuni ya taarifa za mikutano 8(1) ya baraza la madiwani kwa kualika mkutano kabla ya siku moja na pasipo kuwasilisha makablasha kwa madiwani kuhusu kikao hicho huku
wakimtaka aache kuendesha vikao kwa kushinikizwa na mkuu wa wilaya na mkuu wa mkoa .
-Picha zote na Kadama Malunde1 blog


Mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Lewis Kalinjuna akizungumza katika kikao hicho ambapo aliwaeleza madiwani hao kuwa ameitisha kikao cha bajeti kwa haraka kwa ajili ya kujadili na kupitisha bajeti ya halmashauri ya manispaa ya Shinyanga kufuatia ushauri wa sekretariati ya mkoa na kuwahisha taarifa wizara ya fedha.Baada ya kutoa taarifa hiyo ndipo madiwani wakaibua hoja ya kuwa kikao kimeitishwa kwa kukiuka kanuni za vikao vya halmashauri hiyo


Barua ya mualiko wa kikao


Diwani wa kata ya Ndembezi kupitia Chama Cha Mapinduzi David Nkulila akizungumza katika kikao hicho ambapo alisema ni vyema kanuni za halmashauri zikaheshimiwa badala ya kuendesha kikao kwa kuvizia na kwa ubabe kwani ni kutowatendea haki wajumbe wa kikao hicho ambao ni wawakilishi wa wananchi.



Kanuni hiyo inayomtaka mkurugenzi kutoa taarifa kwa maandishi kwa madiwani katika muda usiopungua siku saba kuhusu kikao ikiwa ni pamoja na makablasha ya kikao jambo ambalo mkurugenzi huyo hakulifanya.



Katika katikati ni mkurugenzi wa manispaa ya Shinyanga Lewis Kalinjuna akiteta jambo na mwenyekiti wa kikao hicho ambaye ni naibu meya wa manispaa ya Shinyanga Agnes Machiya aliyelazimika kuahirisha kikao hicho mpaka pale mkurugenzi atakapoitisha kikao kwa kufuata kanuni



Madiwani wakitoka ukumbini baada ya kikao kuahirishwa




Madiwani na watendaji halmashauri ya manispaa ya Shinyanga wakiwa wamepigwa butwa baada ya kikao kuvunjika ghafla




Madiwani wakitoka ukumbini




Diwani bi Zuhura Waziri akitoka ukumbini




Watendaji wa halmashauri ya manispaa ya Shinyanga wakitoka ukumbini




Watendaji
Kikao kimevunjika


Diwani wa kata ya Ndembezi David Nkulila akitoka ukumbini-Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post