Chama cha wananchi CUF kimethibitisha kuandika barua tume ya uchaguzi Zanzibar ya kutaka majina ya wagombea wake wote wa urais, wawakilishi na madiwani yaondoshwe katika orodha ya karatasi za kupiga kura katika uchaguzi wa marudio Machi 20.
Naibu katibu mkuu wa chama hicho Nassor Ahmed Mazrui ametoa kauli hiyo wakati akiongea na wandishi wa habari Zanzibar ambapo amesema ni kweli wamepokea barua ya tume inayowataka wathibitishe na wao tayari wameshatekeleza ombi la barua hiyo kwa kutaka majina yao ya wagombea ikiwemo la Maalim Seif liondolowe kwa vile wameshaamua kutoshirki uchaguzi huo.
Akizumgumzia suala la kwenda mahakamani kupinga amri ya mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Jecha Salum Jecha ya kutangaza marudio amesema pamoja na sheria kuruhusu wao kama CUF hawana imani na mahakama hiyo kwa vile jaji mkuu wa Zanzibar Mhe Omar Othman Makungu ameshatoa msimamo wa mahakama ambao unaonekana kwenda kinyume na katiba na sheria.
Wakati Machi 20 ndiyo siku ya marudio ya uchaguzi huo wazanzibar uliofutwa mwaka jana vyama 14 vilivotangaza kushirki vimekuwa na misimamo tafauti ambapo vyama vyingine vimesema vitashiriki na vingine kuhamua kutoshirki huku tume bado haijatoa tamko lingine lolote hadi sasa.
Via>>ITV
Social Plugin