Mkandarasi wa kampuni ya Nyakarungu CIVIL CONSTRUCTION, Harrison Odila ametiwa nguvuni na jeshi la polisi mjini Nansio wilayani Ukerewe kwa madai ya kushindwa kuwalipa vibarua zaidi ya 100 waliokuwa wanajenga barabara ya Butiriti – Guguyu yenye urefu wa kilometa tano kwa kiwango cha udongo.
Mkandarasi huyo amekamatwa na askari polisi wa kituo cha Nansio akiwa katika ofisi za makao makuu ya halmashauri ya wilaya ya Ukerewe, saa chache baada ya vibarua hao kufanya maandamano ya kudai malipo yao kiasi cha shilingi milioni moja laki mbili na elfu hamsini.
Diwani wa kata ya ngoma ambako barabara hiyo imejengwa na kukamilika tangu mwezi Septemba Mwaka jana Bw.Msingi Musese amelalamikia kitendo kilichofanywa na mkandarasi huyo cha kuwapiga danadana vibarua hao.
Mkuu wa idara ya ujenzi katika halmashauri ya wilaya ya Ukerewe mhandisi mapinduzi Magesa Mwita ambaye ameshuhudia mkandarasi wa kampuni hiyo ya Nyakarungu akitiwa nguvuni na askari polisi wawili alikuwa na haya ya kusema kuhusiana na wakandarasi wenye tabia kama hiyo.
Social Plugin