Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Picha 25 !!WAANDISHI WA HABARI MKOA WA SHINYANGA WATEMBELEA MGODI WA ACACIA BUZWAGI



Hapa ni katika ukumbi wa mikutano wa Mgodi wa Dhahabu wa ACACIA Buzwagi uliopo wilayani Kahama mkoani Shinyanga.Pichani ni Meneja mkuu wa Mgodi wa ACACIA Buzwagi Asa Mwaipopo akizungumza na waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga wakati wa ziara iliyoandaliwa na mgodi huo kwa ajili ya kujionea shughuli za uzalishaji wa madini inavyofanyika.Waandishi wa habari pia walipata fursa ya kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa na mgodi huo katika jamii inayozunguka mgodi huo.Mwaipopo alisema lengo la ziara hiyo ni kuwajengea uwezo waandishi wa habari ili waweze kuandika habari kuhusu mgodi huo kwa usahihi-Malunde1 blog imekusogezea picha kuanzia mwanzo mpaka mwisho wa ziara hiyo,Tazama hapa chini




Kushoto ni Meneja mkuu wa Mgodi wa ACACIA Buzwagi Asa Mwaipopo akizungumza na waandishi wa habari kuhusu namna mgodi unavyofanya kazi na kuelezea kuhusu miradi mbalimbali inayotekelezwa na mgodi huo ambapo kwa mwaka 2015 kuanzia mwezi Januari hadi Desemba jumla ya fedha zilizotumika kwenye miradi pekee ni dola za Kimarekani 1,256,624.48.




Kulia ni mwenyekiti wa Klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga Kadama Malunde akimsikiliza kwa umakini meneja mkuu wa mgodi wa ACACIA Buzwagi Asa Mwaipopo ambaye alisema ziara hiyo itasaidia kwa kiasi kikubwa kuwapa uelewa waandishi wa habari juu ya mazingira ya kazi katika mgodi huo



Mhandisi wa mgodi wa ACACIA Buzwagi Danford Lipenege akieleza namna mgodi huo ulivyopata usajili na kuanza kufanya kazi na namna mgodi huo utakavyofungwa kutokana na gharama kubwa za uzalishaji



Waandishi wa habari wakiwa ukumbini,kushoto ni Afisa Mahusiano wa mgodi wa ACACIA Buzwagi Magesa Magesa



Kulia ni Mhandisi wa mgodi wa ACACIA Buzwagi Danford Lipenege wakati akizungumza na waadishi wa habari,kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano katika mgodi wa ACACIA Buzwagi Blandina Munghezi,katikati ni Marco Peter afisa kutoka ACACIA Buzwagi



Hili ni shimo lenye urefu wa mita 210 ambamo madini ya dhahabu yanachimbwa katika mgodi huo



Afisa Mazingira katika mgodi wa ACACIA Buzwagi Frank Ngoroma akitoa maelezo kwa waandishi wa habari jinsi madini yanavyochimbwa katika mgodi huo



Afisa Mazingira katika mgodi wa ACACIA Buzwagi Frank Ngoroma akiendelea kutoa maelekezo kwa waandishi wa habari,kushoto ni Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano katika mgodi wa ACACIA Buzwagi Blandina Munghezi



Kiongozi wa bwawa la kuhifadhia maji yenye sumu(nyuma) katika mgodi wa ACACIA Buzwagi Yona Ernest Mshanga akieleza namna wanavyotunza maji hayo ili yasiende kwenye makazi ya watu,ambapo alisema wanafanya kazi kwa tahadhali kubwa na maji hayo yanatunzwa katika chombo ambacho hayawezi kuvuja



Mkuu wa Kitengo cha Mawasiliano katika mgodi wa ACACIA Buzwagi Blandina Munghezi akiwa na mwandishi wa habari gazeti la Nipashe Mohab Dominic katika bwawa la kuhifadhia maji yenye sumu katika mgodi huo,nyuma yao ni waandishi wa habari




Afisa Mazingira katika mgodi wa ACACIA Buzwagi Frank Ngoroma akiongozana na waandishi wa habari kutembelea maeneo mbalimbali katika mgodi huo,kulia kwake ni mwandishi wa habari gazeti la Mwananchi Shija Felician



Hili ni bwawa la maji masafi katika mgodi wa ACACIA Buzwagi yanayozalishwa katika mgodi huo,lakini pia maji ya mvua na kutoka ziwa Victoria



Waandishi wa habari wakiwa karibu na bwawa la maji masafi katika mgodi wa ACACIA Buzwagi



Waandishi wa habari wakiwa karibu na bwawa la maji masafi katika mgodi huo



Afisa Mazingira katika mgodi wa ACACIA Buzwagi Frank Ngoroma akisisitiza jambo,katikati ni Afisa Mahusiano wa mgodi wa ACACIA Buzwagi Magesa Magesa,kushoto ni mwandishi wa habari gazeti la Nipashe Mohab Dominic





Afisa mtendaji wa kata ya Mwendakulima iliyopo karibu na mgodi wa ACACIA Buzwagi Mussa Ibingo akiwa katika mradi wa kisima cha maji katika kata hiyo,ambapo kwa mujibu wa afisa mahusiano wa mgodi wa huo Moses Msofe(aliyesimama kulia) katika kata hiyo kuna visima virefu 16 vilivyojengwa na mgodi huo





Hiki ni kutuo cha afya cha Mwendakulima kilichojengwa na mgodi wa ACACIA Buzwagi,tayari kimeshaanza kutoa huduma za afya




Muuguzi msaidizi katika Kituo cha afya Mwendakulima Celestina Mbezi akionesha kitanda cha kujifungulia kwa akina mama



Hii ni shule ya msingi Budushi katika kata ya Mwendakulima inayoendelea kujengwa na mgodi wa ACACIA Buzwagi



Afisa mahusiano wa mgodi wa huo Moses Msofe akionesha matofali ya kufungamana yaliyotengenezwa na vijana 60 kutoka kata ya Nyahanga na Mwendakulima waliopewa elimu ya ujasiriamali na mgodi huo



Hii ni Nyumba ya walimu wa shule ya msingi Mwime katika kata ya Mwendakulima ambayo imejengwa na mgodi wa ACACIA Buzwagi



Hiki ni choo cha kisasa kilichojengwa katika shule ya msingi Mwime,ikiwa ni miongoni shule 6 za msingi kata ya Mwendakulima ambazo ni Mwime, Chapulwa, Budushi, Busalala, Mwendakulima na Mwendakulima B zilizojengewa mashimo 16 ya vyoo kila shule katika mradi wa vyoo kutoka mgodi wa ACACIA Buzwagi




Meneja mkuu wa mgodi wa ACACIA Buzwagi Asa Mwaipopo akizungumza na waandishi wa habari baada ya kumaliza ziara yao katika mgodi huo kwa kuangalia mazingira ya kazi na miradi inayotekelezwa na mgodi huo,ambapo


aliishukuru serikali ya wilaya ya Kahama kwa ushirikiano wanaoutoa katika kutekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwemo ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami,miradi ya elimu,afya,maji na utaratibu wa kuwapatia elimu ya ujasiriamali wananchi wanaoishi jirani na mgodi huo.



Mwaipopo alisema kuanzia mwezi Januari hadi Desemba mwaka 2015 jumla ya fedha zilizotumika kwenye miradi pekee ni dola za Kimarekani 1,256,624.48.




Kushoto ni mwenyekiti wa klabu ya waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga Kadama Malunde na katibu mtendaji wa klabu hiyo Stephen Wang'anyi wakiteta jambo na meneja mkuu wa mgodi wa ACACIA Buzwagi Asa Mwaipopo baada ya kumaliza ziara yao katika mgodi huo


Waandishi wa habari mkoa wa Shinyanga wakiwa katika picha ya pamoja na meneja mkuu wa mgodi wa ACACIA Buzwagi Asa Mwaipopo-Picha zote na Kadama Malunde na Mohab Dominic

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com