Msimamizi mkuu wa uchaguzi wa mwenyekiti
wa Chama Cha Mapinduzi(CCM) mkoa wa Shinyanga leo ndugu Abdalah Bulembo
ambaye ni mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi CCM taifa akizungumza katika
Uwanja wa CCM Kambarage mjini Shinyanga leo baada ya uchaguzi wa awamu
ya kwanza ambapo wagombea walipata kura ambazo hazifiki nusu ya wajumbe
wa halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Shinyanga waliopiga kura.Bulembo
alitangaza uchaguzi urudiwe,Wagombea wa kiti hicho walikuwa watatu ambao
ni Hassan Mwendapole aliyepata kura 21,Mabala Mlolwa kura 395 na Erasto
Kwilasa kura 384 katika uchaguzi wa awamu ya kwanza-Fuatilia hapa chini
Matukio yaliyojiri-Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog Shinyanga
Masanduku ya kupigia kura yakiwa tayari kwa ajili ya uchaguzi wa awamu
ya pili leo,ambapo msimamizi wa uchaguzi huo Abdalah Bulembo alisema
mgombea aliyepata kura chache zaidi katika uchaguzi wa awamu ya kwanza
hatahusika katika uchaguzi wa awamu ya pili badala yake wagombea
watakuwa wawili tu ambao ni Kwilasa na Mlolwa
Wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Shinyanga wakiwa katika foleni ya kupigia kura
Tunasubiri kupiga kura...
Wakati zoezi la kupiga kura linaendelea Mvua ilianza kunyesha...zoezi likasitishwa kwa muda....
Wajumbe wa halmashauri kuu ya CCM mkoa wa Shinyanga wakisubiri mvua ikatike ili waendelee na zoezi la kupiga kura
Maboksi ya kupigia kura yakaondolewa kwenye mvua na kulindwa
Meza kuu ikawa haikaliki kutokana na mvua kuendelea kunyesha
Wapiga kura wengine wakaamua kukimbilia kwenye jukwaa kuu la uwanja wa CCM Kambarage kwa ajili ya kujikinga na mvua
Ilikuwa mvua ya upepo lakini wenye roho ngumu wakavumilia kwenye mabanda
yaliyokuwa uwanjani hapo huku waliokuwa kwenye jukwaa la uwanja nao
wakilowana pamoja na kwamba waliamini kuwa watajikinga na mvua
Hata kabla ya matokeo kutangazwa tayari Wanaccm walikuwa wameanza
kusherehekea,hatukujua kama ni muziki mnene wa nyimbo za CCM ama pengine
walikuwa wameshajua nani kashinda nafasi hiyo ya uenyekiti wa CCM mkoa
wa Shinyanga
Tunasubiri matokeo yatangazwe....
Kada wa CCM akicheza kabla ya matokeo kutangazwa
Makada wa CCM wakiteta jambo wakati wanasubiri matokeo yatangazwe
Wanacheza na kushangilia kabla ya matokeo kutangazwa
Muda Ukawadia...Msimamizi wa uchaguzi Abdalah Bulembo akitangaza matokeo
ya uchaguzi huo,ambapo alisema jumla ya wajumbe wa kamati kuu ya CCM
mkoa wa Shinyanga waliopiga kura katika uchaguzi wa pili ni 814,kura
zilizoharibika ni tano,kura halali zilizopigwa ni 809,ambapo alimtangaza
Kwilasa kushinda kwa kura 427 huku Mabala akiambulia kura 382.
Kwilasa anachukua nafasi ya Khamis Mgeja aliyetimukia Chadema mwezi
Sepetemba 2015 wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu kwa madai kuwa CCM
imekosa mwelekeo.Kwilasa ataongoza chama hicho kwa muda wa mwaka mmoja
na nusu kabla ya kufanyika uchaguzi mwingine nchi nzima kutafuta
wenyeviti wa mikoa.
Kushoto ni ndugu Mabala Mlolwa ambaye akizungumza baada ya matokeo
kutangazwa,ambapo alisema amekubali matokeo na kuahidi kumpa ushirikiano
mwenyekiti mpya wa CCM mkoa wa Shinyanga
Kulia ni msimamizi wa uchaguzi Abdalah Bulembo akimkaribisha mwenyekiti
mpya wa CCM mkoa wa Shinyanga ndugu Erasto Kwilasa(kushoto),Bulembo
alimpongeza Kwilasa kwa ushindi huo na kumtaka kufanya kazi kwani sasa
ni Hapa Kazi tu
Mwenyekiti mpya wa CCM mkoa wa Shinyanga Erasto Kwilasa akiwashukuru
wapiga kura kwa kumchagua kuwa mwenyekiti wa CCM mkoa wa
Shinyanga,ambapo aliahidi kuondoa makundi ndani ya chama hicho
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Erasto Kwilasa akizungumza na
wanachama wa CCM katika uwanja wa CCM Kambarage huku msimamizi wa
uchaguzi huo Abdalah Bulembo akisikiliza kwa umakini maneno ya Kwilasa
Makada wa CCM wakiwa eneo la tukio
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Erasto Kwilasa akizungumza baada ya ushindi
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Erasto Kwilasa akisisitiza jambo
Hapakuwa na muda tena wa kucheza wala kushangilia ushindi..Mwenyekiti wa
CCM mkoa wa Shinyanga Erasto Kwilasa anaondoka uwanjani baada ya kutoa
hotuba fupi
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Shinyanga Erasto Kwilasa akiondoka uwanjani
Makada wa CCM wakisukumagari la mwenyekiti mpya wa CCM mkoa wa Shinyanga Erasto Kwilasa.
Kwilasa anayetokea katika wilaya ya Shinyanga alikuwa anachuana na
Mabala Mlolwa kutoka wilaya ya Kahama na Hassan Mwendapole kutoka wilaya
ya Shinyanga,ambapo Mabala alipata kura 382 katika uchaguzi wa awamu ya
pili baada ya kura za uchaguzi wa awamu ya kwanza mshindi kutovuka nusu
ya kura zote.
Katika uchaguzi wa awamu ya kwanza Kwilasa alipata kura 384,Mabala
Mlolwa kura 395 huku Hassan Mwendapole akipata kura 21 hali iliyopelekea
Msimamizi wa Uchaguzi huo Abdalah Bulembo ambaye ni mwenyekiti wa
Jumuiya ya wazazi CCM taifa kutangaza uchaguzi urudiwe kwa wagombea
wawili ambao ni Erasto Kwilasa na Mabala Mlowa.
Uchaguzi wa awamu ya pili ulimalizika kwa kumfanya Kwilasa kumbwaga
chini Mabala aliyekuwa ameongoza katika uchaguzi wa awamu ya kwanza.
Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog Shinyanga