Hpa ni katika ukumbi wa mikutano wa Katemi Hotel katika eneo la Ngokolo Mitumbani mjini Shinyanga ambako kumefanyika
warsha ya siku mbili ya kufanya tathmini ya mpango mkakati wa TGNP Mtandao wa kuwajengea uwezo wanawake,vijana na watu wenye ulemavu kushiriki katika uchaguzi wa serikali za mitaa mwaka 2014 na uchaguzi mkuu mwaka 2015 iliyofanyika mjini Shinyanga.Washiriki wa warsha hiyo wametoka katika mikoa ya Shinyanga,Mara na Simiyu.Washiriki wametumia fursa hiyo kujadili changamoto walizokabiliana nazo wanawake,vijana na watu wenye ulemavu katika uchaguzi uliopita na kujadili mikakati mbalimbali ya kufanikisha malengo yao katika chaguzi zijazo.
Mwandishi mkuu wa Malunde1 blog,ndugu Kadama Malunde amehudhuria warsha hiyo,ametuletea picha zifuatazo.....
Siku ya Kwanza-Februari 04,2016-Mwezeshaji wa warsha hiyo Dinah Nkya kutoka TGNP Mtandao akizngumza wakati wa ufunguzi wa warsha hiyo ambapo alisema lengo kuu la warsha mrejesho hiyo ni kupima utekelezaji wa mpango kazi waliojiwekea washiriki baada ya mafunzo ya awali yaliyoanza mwaka 2014 kwa kuangalia namna walivyotumia nafasi zao,ushawishi wao katika kuelimisha jamii kuhusu ushiriki wa wanawake,vijana na walemavu katika mchakato wa uchaguzi na uongozi wa siasa.
Baadhi ya Washiriki kutoka mkoani Mara wakifuatilia kilichokuwa kinajiri ukumbini
Baadhi ya washiriki kutoka wilaya ya Kahama wakiwa ukumbini
Baadhi ya washiriki kutoka manispaa ya Shinyanga wakiwa ukumbini
Washiriki wakiwa ukumbini
Washiriki wakifuatilia kilichokuwa kinajiri ukumbini
Mwezeshaji kutoka TGNP Mtandao Rebeca Mjema Kisena akizungumza katika warsha hiyo ambapo alisema katika uchaguzi mkuu 2015 wa madiwani,wabunge na rais kumekuwa na ongezeko la wanawake,vijana na watu wenye ulemavu katika nafasi za ubunge na udiwani kutokana na mradi wa uchaguzi wa TGNP mwaka 2014/2016 wa kuhamasisha makundi hayo kushiriki katika chaguzi mbalimbali
Washiriki katika warsha hiyo wakifuatilia kilichokuwa kinajiri ukumbini
Mwandishi wa habari kutoka Radio Faraja Moshi Ndugulile akiwa ukumbini
Kushoto ni Mwezeshaji msaidizi kutoka TGNP Mtandao Ernest Mpalile akijaza dodoso wakati wa mahojiano na mmoja wa washiriki wa warsha hiyo ,Veronica Natalis kuhusu namna alivyoshiriki katika kutekeleza mradi wa uchaguzi
Kushoto ni Mwezeshaji wa warsha hiyo Dinah Nkya kutoka TGNP Mtandao akifanya mahojiano na mshiriki wa warsha hiyo Bonny Matto kutoka Tarime mkoani Mara
Siku ya Pili ya warsha Februari 05,2016-Wawezeshaji katika warsha hiyo kutoka TGNP wakiteta jambo ukumbini
Washiriki wa warsha hiyo wakifanya kazi za makundi
Mjadala unaendelea
Waandishi wa habari wakiwa ukumbini
Kushoto ni Mwezeshaji msaidizi kutoka TGNP Mtandao Ernest Mpalile
Washiriki wakiimba wimbo kuhusu usawa wa kijinsia
Tunaimba wimbo......
Washiriki wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea ukumbini
Marco Mkanjiwa,ambaye ni mwenyekiti wa Shirikisho la watu wenye ulemavu wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga akizungumza ukumbini
Mraghabishi kutoka shirika la Sheria na Haki za Binadamu Tarime mkoani Mara ,Bonny Matto akiwa ukumbini
Mwezeshaji kutoka TGNP Mtandao Rebeca Mjema Kisena akizungumza ukumbini
Tunafuatilia kinachoendelea ......
Warsha inaendelea
Bwana Iddy Mpyalimi akichangia mada ukumbini
Mwandishi wa habari Moshi Ndugulile akieleza namna vyombo vya habari vilivyotumika kuhamasisha wanawake,vijana na walemavu kushiriki katika uchaguzi mkuu mwaka 2015
Mwandishi wa habari Masanja akizungumza ukumbini
Mkurugenzi wa Malunde1 blog,Fahari ya Shinyanga,bwana Kadama Malunde,akiwa ukumbini
Kulia ni bwana Marco Maduhu mwandishi wa habari gazeti la Nipashe akiwa na bwana Frank Mshana mwandishi wa habari ITV na Radio One
Washiriki wakiwa katika kazi ya kikundi
Washiriki wakiwa katika kazi ya kikundi
Kazi za makundi zinaendelea
Washiriki wakiwa katika kazi ya kikundi
Wawezeshaji wakiteta jambo ukumbini,kulia ni Dinah Nkya akiwa na Rebeca Mjema
Washiriki wakiimba ukumbini
Wawezeshaji na washiriki wa warsha hiyo wakiimba na kucheza ukumbini
Mshiriki wa warsha hiyo Marry kutoka manispaa ya Shinyanga akiwasilisha kazi ya kundi lake
Mratibu wa warsha hiyo bi Janeth Mawinza akizungumza ukumbini
Bwana Masanja kutoka mkoani Simiyu akiwasilisha kazi ya kundi lake
Bwana Bonny Matto kutoka mkoani Mara akiwasilisha kazi ya kundi lake
Kushoto ni mwezeshaji msaidizi kutoka TGNP Elieth Samwel Eliyuko,akifuatiwa na mwezeshaji msaidizi Ernest Mpalile na mratibu wa warsha hiyo Janeth Mawinza
Picha ya pamoja baada ya warsha kumalizika Februari 05,2016
Picha ya pamoja washiriki wote
Picha ya pamoja- Picha zote na Kadama Malunde- Malunde1 blog Shinyanga
Social Plugin