Wafanyakazi kumi na tatu wa kampuni ya Kyaka Ranching inayomiliki kitalu cha ufugaji namba kumi na sita kilichoko eneo la Kagoma lililoko mkoani Kagera kilichobinafsishwa kampuni ya ranchi ya taifa (NARCO) wamenusika kifo baada ya kukatwa katwa na mapanga na kundi la wafugaji waliokuwa na silaha mbalimbali walipovamia kambi ya kampuni hiyo kwa lengo la kufanya hujuma baada ya walinzi wa kampuni hiyo kuwazuia kuingiza mifugo yao kwa nguvu kwenye kitali hicho.
Wafugaji hao walivamia kambi hiyo usiku wa kuamkia jana huku silaha mbalimbali ambazo ni pamoja na mapanga, visu, marungu na mishale ambazo ndizo walizitumia kuwajeruhi baadhi ya wafanyakazi hao kwa kuwakatakata mapanga kwenye sehemu mbalimbali za miili yao na katika kufanya uvamizi huo walimnyanganya mlinzi wa kampuni hiyo bunduki aina ya shortgun na kuondoka nayo.
Pia walifanya uharibifu mkubwa wa mali ambazo ni pamoja na kuvunja vioo vya madirisha na milango ya jengo la utawala na nyumba za wafanyakazi na kuiba mali, pia waliondoka na ngombe arobaini na nane na kuharibu vioo vya gari moja na pikipiki tatu ambazo hutumiwa na wafanyakazi kufanya doria na kubeba maji, Samwel Sylvester ni miongoni wafanyakazi waliojeruhiwa vibaya waliolazwa hospitali ya Nyakahanga.
Kwa upande wake, Patric Ishengoma mkurugenzi wa kampuni ya Kyaka Ranching, inayomiliki kitalu namba kumi na sita kilichovamiwa akizungumzia juu ya tukio hilo, amesema hujuma zinazofanywa na wafugaji wanaoingiza ngombe wao kwa nguvu kwenye vitalu wananvyovimiliki kuwa zinawakatisha tamaa wawekezaji waliomilikishwa vitalu kwa ajili ya ufugaji wa kisasa hasa wanaotumia mitaji mikubwa katika kuendeleza vitalu hiyo, hivyo ameiomba serikali kutafuta namna ya kutatua tatizo kati yao na wanaovamia vitalu vyao.
Naye, kamanda wa jeshi la polisi mkoani kagera augustine ullomi amethibitisha kutokea kwa tukio hilo, amesema kwa sasa jeshi la polisi linawashikilia watu kwa kuhusika na tukio hilo akiwemo mlinzi wa kampuni hiyo aliyenyanganywa bunduki na linaendelea kuwasaka watu wengine waliokimbia.
Social Plugin