Wanawake zaidi ya 450 nchini hupoteza maisha wakati wa kujifungua kati ya vizazi hai laki moja kwa mwaka vinavyosababishwa na huduma mbovu za afya ya uzazi, vifaatiba, uhaba wa wakunga na wauguzi katika vituo vya afya na hospitalini pamoja na ubovu wa miundombinu ya barabara.
Akitoa takwimu hizo kwenye mkutano uliohusisha wakunga na wauguzi wa mikoa na wilaya hapa nchini meneja miradi Amref Tanzania Dokta Piusi Chaya amesema kufuatia vifo hivyo na changamoto ya uhaba wa wauguzi shirika hilo limejetolea kusomesha wauguzi 254 kwa ngazi ya cheti huku wengine 80 wamehitimu masomo yao na tayari wamerejea katika vituo vyao vya kazi.
Kwa upande wao baadhi ya wakunga na wauguzi wakuu wa mikoa wamesema wanakabiliwa na changamoto nyingi zinazokwamisha utenda na kuwahudumia wanawake wajawazito na kuokoa maisha yao wakati wa kujifungua na hapa wanaeleza.
Social Plugin