AGPAHI YAKUTANA NA WATU WANAOISHI NA VVU MKOA WA SIMIYU WANAOTOA HUDUMA KWENYE VITUO VYA TIBA NA MATUNZO



Hapa ni katika ukumbi wa KKKT mjini Bariadi mkoani Simiyu ambapo Shirika la Kitanzania lisilo la kiserikali la Ariel Glaser Pediatric Aids Healthcare Initiative( AGPAHI) linalojihusisha na mapambano dhidi ya Virusi Vya Ukimwi (VVU) na UKIMWI limekutana na watu wanaoishi na maambukizi ya Virusi vya Ukimwi katika mkoa wa Simiyu wanaosaidia kuwaunganisha wateja na Vituo vya kutoa huduma za tiba na Matunzo kwa watu wanaoishi na VVU (WAVIU Washauri) katika warsha ya siku tatu.


Warsha hiyo imefanyika kuanzia Machi 17 hadi Machi 19,2016 ikiwa na kuwajengea uwezo WAVIU Washauri ili waweze kuwaunganisha wateja kutoka kwenye jamii kwenda kwenye vituo vya tiba na matunzo na kuwafuatilia wateja waliopotea katika huduma na kuwarudisha pia kuainisha changamoto zinazosababisha wateja wasifike kwenye huduma na kutafuta njia sahihi za kutatua changamoto hizo .

Pichani ni Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa jamii kutoka Shirika la AGPAHI, Richard Kambarangwe anayesimamia mkoa wa Simiyu akifungua warsha ya WAVIU Washauri kutoka halmashauri za wilaya za mkoa wa Simiyu,Bariadi mjini,Bariadi vijijini,Maswa,Meatu,Itilima na Busega.Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog



Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa jamii kutoka Shirika la AGPAHI, Richard Kambarangwe alitumia fursa hiyo kuwataka watu waliopata maambukizi ya VVU kuendelea kutumia dawa za kufubaza makali ya VVU na kutoa elimu kwa jamii kuhusu VVU na UKIMWI huku akiwasihi WAVIU washauri kutoa huduma nzuri kwa wateja katika vituo vya tiba na Matunzo wanakofanyia kazi.



Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa jamii kutoka Shirika la AGPAHI, Richard Kambarangwe aliwataka pia WAVIU washauri kuunda vikundi vya watoto na watu wazima katika CTC zao zitakazorahisisha utoaji wa huduma kwa watu waliopata maambukizi ya VVU.
 
Kambarangwe aliwahamasisha WAVIU Washauri kutumia mbinu mbalimbali kuwarudisha kwenye huduma ya kutumia dawa wateja walioacha kutumia dawa za kufubaza makali ya VVU



Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa jamii kutoka Shirika la AGPAHI, Cecilia Yona anayesimamia mkoa wa Shinyanga akielezea historia ya shirika la AGPAHI na mikakati yake katika kupambana na VVU na UKIMWI



WAVIU washauri kutoka mkoa wa Simiyu wakifuatilia maelezo ya Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa jamii kutoka Shirika la AGPAHI, Cecilia Yona



Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa jamii kutoka Shirika la AGPAHI, Cecilia Yona akizungumza katika ukumbi wa KKKT mjini Bariadi mkoani Simiyu wakati wa warsha kwa WAVIU Washauri iliyoandaliwa na shirika la AGPAHI



WAVIU Washauri kutoka Simiyu wakifanya kazi ya kikundi juu ya ushauri nasaha na upimaji wa damu kwa hiari



Mwezeshaji katika warsha hiyo Gladness Olotu ambaye ni muuguzi msaafu kutoka jijini Mwanza aliyebobea katika fani ya Ushauri nasaha akitoa elimu ya ushauri nasaha



Hapa ni washiriki wa warsha hiyo wakiwa katika jengo la kitengo cha tiba na matunzo kwa watu wanaoishi na VVU(CTC) katika hospitali ya halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu



Washiriki wa warsha hiyo wakiwa katika jengo la kitengo cha tiba na matunzo (CTC) Hospitali ya wilaya mji Bariadi



MVIU mshauri Happness Malamala katika CTC ya hospitali ya mji wa Bariadi akiwaeleza WAVIU washauri kutoka wilaya za mkoa wa Simiyu namna ya kupanga mafaili ya wateja ili kuepuka kupoteza kumbukumbu muhimu



Mafaili ya wateja katika CTC ya hospitali ya halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu yakiwa katika mpangilio mzuri



Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa jamii kutoka Shirika la AGPAHI, Richard Kambarangwe akizungumza katika CTC hiyo ambapo aliwasisitiza WAVIU washauri kutunza vizuri taarifa za wagonjwa ili kurahisisha kazi ya kuwatafuta watoro katika tiba



WAVIU washauri wakifuatilia kilichokuwa kinaendelea



Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa jamii kutoka Shirika la AGPAHI, Richard Kambarangwe akizungumza katika CTC ya hospitali ya halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu



MVIU mshauri Happness Malamala kieleza namna anavyofanya kazi zake katika CTC ya hospitali ya halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu

.

Muuguzi katika ya hospitali ya halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu Catherine Mwangi akionesha dawa za kufubaza makali ya VVU,kulia kwake ni Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa jamii kutoka Shirika la AGPAHI, Richard Kambarangwe



Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa jamii kutoka Shirika la AGPAHI, Richard Kambarangwe kutoka mkoa wa Simiyu akiwa na Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa jamii kutoka Shirika la AGPAHI, mkoa wa Shinyanga Cecilia Yona wakitoka katika CTC ya hospitali ya halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu



WAVIU washauri wakiondoka katika hospitali ya halmashauri ya mji wa Bariadi mkoani Simiyu baada ya kutembelea CTC hiyo kujifunza namna huduma zinavyotolewa katika kituo hicho cha tiba na matunzo



Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa jamii kutoka Shirika la AGPAHI, Richard Kambarangwe akielezea juu namna ya kutumia kitabu cha usajili wa wateja katika CTC



Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa jamii kutoka Shirika la AGPAHI, Richard Kambarangwe akielezea juu namna ya kutumia vitabu vya miadi na ufuatiliaji katika CTC



Kulia ni MVIU Mshauri Nhandi Bulengela kutoka CTC ya hospitali ya Mkula katika wilaya ya Busega anayeishi na VVU tangu mwaka 2003 akichangia mada ambapo aliiomba serikali kuungana na shirika la AGPAHI kutoa elimu kwa waganga wa jadi juu ya VVU na UKIMWI.

Kulia ni Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa jamii kutoka Shirika la AGPAHI, Cecilia Yona akisikiliza kwa umakini maelezo ya Bulengela..Bulengela alisema Ukimwi unaua kama hautalikubali tatizo lakini ukishakubali matokeo na kufuata masharti ya dawa utaishi miaka mingi hivyo kuwataka watu waliopata maambukizi kulikubali tatizo hilo na kuelimisha jamii juu ya VVU na UKIMWI



Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa jamii kutoka Shirika la AGPAHI, Cecilia Yona akiwasisitiza WAVIU Washauri kufuatilia wateja waliopotea katika huduma ya tiba na matunzo



MVIU mshauri kutoka kituo cha Lugulu kilichopo wilaya ya Itilima mkoani Simiyu Faustine Maige akitoa ushuhuda namna alivyopata maambukizi ya VVU miaka kadhaa iliyopita.Alisema bado kuna watu katika jamii hawaamini kuwa wamepata maambukizi ya VVU matokeo yake wanakimbilia kwa waganga wa jadi.Maige alieleza pia namna walivyofanikiwa kuanzisha vituo vya watoto na watu wazima wanaoishi na VVU kwa ajili ya huduma ya tiba na matunzo




MVIU Mshauri Chagu Hamis kutoka CTC ya hospitali ya wilaya ya Maswa mkoani Simiyu akizungumza katika warsha hiyo ambapo alisema dawa pekee ya kupambana na Ugonjwa wa Ukimwi kwa watu waliopata maambukizi ya Virusi vya Ukimwi ni watumiaji wa dawa za kufubaza makali ya VVU ni kuwa mfuasi mzuri wa dawa hizo hali itakayomfanya mtumiaji aishi duniani kwa miaka mingi zaidi.

Hamis ambaye anaishi na virusi vya Ukimwi tangu mwaka 2012 alisema baadhi ya watu wanaoishi na VVU wamekuwa wakipuuza kutumia dawa za kupunguza makali ya VVU matokeo yake miili yao inadhoofika na kusababisha wakati mwingine kufariki dunia.




MVIU Mshauri kutoa CTC ya Nkololo iliyopo Bariadi Vijijini Bi Magreth Masalu akitoa ushuhuda na historia yake katika matumizi ya Dawa za kufubaza makali ya VVU



Kushoto ni Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa jamii kutoka Shirika la AGPAHI, Richard Kambarangwe akizungumza wakati wa kufunga warsha hiyo iliyodumu kwa muda wa siku tatu



Mganga mkuu wa mkoa wa Simiyu Dkt Mageda Kilulya akifunga warsha ya WAVIU Washauri wa mkoa wa Simiyu.Dkt Kilulya alisema ili kukabiliana na wateja wengi wanaopotea katika huduma, mkoa wake kwa kushirikiana na shirika la AGPAHI wamekuwa wakitoa elimu kwa WAVIU Washauri na watu wanaoishi na VVU na UKIMWI juu ya madhara ya kutotumia dawa za kupunguza makali ya VVU.



Dkt Kilulya alisema hivi sasa wanaendelea kutoa pia elimu kwa waganga wa kienyeji juu ya VVU na Ukimwi ili kusaidia wateja walioanza kutumia dawa warudi kwenye huduma huku akiongeza kuwa mkoa wa Simiyu hauna tatizo la upungufu wa dawa aina ya Septrini kwa ajili ya watu waliopata maambukizi ya VVU lakini wanakinga kubwa mwilini hawajaanza kutumia dawa za ARV’S/ART.

Picha zote na Kadama Malunde-Malunde1 blog


BONYEZA MANENO HAYA KUANGALIA PICHA ZA WARSHA YA WAVIU MKOA WA SHINYANGA

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post