Mwenyekiti wa Kamati ndogo ya Sheria za Uratibu wa Kuandaa na Kuchapishwa kwa sheria ndogo ndogo za Bunge Mhe. William Ngeleja (kushoto) akizungumza na wajumbe wa kamati hiyo (hawapo pichani) wakati wa ziara yake katika Idara ya Mpigachapa Mkuu wa Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu Machi, 15, 2016 wa kwanza kulia ni Mpigachapa Mkuu wa Serikali Bw.Cassian Chibogoyo.
Mwenyekiti wa Kamati ndogo ya Sheria za Uratibu wa Kuandaa na Kuchapishwa kwa sheria ndogo ndogo za Bunge Mhe. William Ngeleja (katikati) akiwa katika ziara yake katika Idara ya Mpigachapa Mkuu wa Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu Machi, 15, 2016.
Mwenyekiti wa Kamati ndogo ya Sheria za Uratibu wa Kuandaa na Kuchapishwa kwa sheria ndogo ndogo za Bunge Mhe. William Ngeleja akielezea umuhimu wa kuhifadhi nyaraka za serikali wakati wa ziara yake katika Idara ya Mpigachapa Mkuu wa Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu Machi 15, 2016 wa kwanza kulia ni Mpigachapa Mkuu wa Serikali Bw.Cassian Chibogoyo.
Mbunge wa Manyoni Mashariki Mhe.Daniel Mtuka akiangalia moja ya kitabu kilichochapishwa na Idara ya Mpigachapa Mkuu wa Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu wakati wa ziara ya Kamati ndogo ya Sheria za Uratibu wa kuandaa na kuchapishwa kwa sheria ndogo ndogo za bunge, wa kwanza kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Uchapishaji Bi.Joyce Benjamin.
Mjumbe wa Kamati ndogo ya Sheria za Uratibu wa Kuandaa na Kuchapishwa kwa sheria ndogo ndogo za bunge Mhe. Halima Mdee (mb) akichangia hoja wakati wa kikao cha kamati hiyo katika Ukumbi wa Idara ya Mpigachapa Mkuu wa Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu Machi 15, 2016.
Katibu Mkuu Sera na Uratibu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Hamis Mwinyimvua (kulia) akimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati ndogo ya Sheria za Uratibu wa Kuandaa na Kuchapishwa kwa sheria ndogo ndogo za bunge Mhe. William Ngeleja wakati wa ziara ya kamati hiyo katika Idara ya Mpigachapa Mkuu wa Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu Machi 15, 2016.
Katibu Mkuu Sera na Uratibu Ofisi ya Waziri Mkuu Dkt. Hamis Mwinyimvua (wa sita kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Kamati ndogo ya Sheria za Uratibu wa kuandaa na kuchapishwa kwa sheria ndogo ndogo za Bunge pamoja na baadhi ya wafanyakazi wa Idara ya Mpigachapa Mkuu wa Serikali Ofisi ya Waziri Mkuu, mara baada ya ziara ya kamati hiyo Machi 15, 2016.(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)