Kulia ni Rais na mtendaji mkuu wa EGPAF, Charles Lyons akiongea na kikundi cha akina mama wanaofaidika na huduma za EGPAF katika kituo cha afya cha USA Rivier mjini Arusha.
Lyons aliwapongeza akina mama hao kwa kutumia fursa waliyoipata katika kuhakikisha wanazuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa watoto wao.
Lyons alisema, yeye pamoja na bodi ya wakurugenzi wa EGPAF imefurahi kupata fursa ya kuadhimisha siku ya wanawake duniani kwa kushuhudia mafanikio ya mradi wa kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto (PMTCT) unaotekelezwa na EGPAF Tanzania kwa kupitia ufadhili wa Serikali ya watu wa Marekani.
“ Mimi binafsi , pamoja na bodi ya wakurugenzi wa EGPAF tumefurahi sana kuadhimisha siku ya wanawake kwa kushuhudia jinsi akimama mnaopata huduma katika kituo cha afya Usa River mlivyoweza kushikamana na kuhakikisha mnazuia maambukizi ya VVU kwa watoto wenu. Hili ni jambo zuri na la kujivunia”,alisema Lyons
Aidha Lyons aliwahamasisha akina mama hao kuendelea na mshikamano na kusaidiana ili kuhakikisha wanatumia dawa za ART vizuri na kuwakinga watoto wao dhidi ya maambukizi ya VVU.
Bi. Sara Steffens, mmoja wa wanachama wa bodi ya EGPAF akiongea na mama katika wodi ya wazazi ya kituo cha afya Ngarenaro , Arusha ambayo baadhi ya huduma zake zinafadhiliwa na Shirika la EGPAF kupitia msaada wa Serikali ya Watu wa Marekani.
Mkurugenzi mtendaji wa KCMC Dr.Gileard Masenga akiikaribisha bodi ya Wakurugenzi wa EGPAF katika hospitali ya KCMC mkoani Kilimanjaro.
Balozi wa EGPAF mkoani Kilimanjaro, Eric Shayo akitoa ushuhuda wa jinsi ambavyo utumiaji mzuri wa dawa za kupunguza makali ya VVU ( ART) umeweza kuimarisha afya yake.
Alilishukuru shirika la EGPAF kwa kuweza kusaidia upatikanaji wa huduma hizo katika mkoa wa Kilimanjaro.
Baadhi ya vijana wanaofaidika na huduma za EGPAF katika kitengo cha kuhudumia wana familia kilichopo hospitali ya KCMC wakionyesha vipaji vyao kwa bodi ya Wakurugenzi pamoja na wafanyakazi wa EGPAF.
Baadhi ya vijana wanaofaidika na huduma za EGPAF katika kitengo cha kuhudumia wana familia kilichopo hospitali ya KCMC wakionyesha vipaji vyao kwa bodi ya Wakurugenzi pamoja na wafanyakazi wa EGPAF.
Vijana hao wamelishukuru shirika la EGPAF kwa kutoa msaada wa dawa na kisaikolojia unaowawezesha kukua wakiwa na afya zilizoimarika. Vijana hao pia wamewaasa watu wanaoishi na VVU kuhakikisha wanafuata ushauri wanaopewa na wataalamu wa afya na kutumia dawa za ART bila kuacha.
Baadhi ya wafanyakazi wa EGPAF wakiwa na bodi ya wakurugenzi ya EGPAF katika ofisi za EGPAF mjini Moshi.
Sambamba na maadhimisho ya siku ya mwanamke duniani, bodi hiyo pia ilipata fursa ya kutembelea hospitali ya Kilimanjaro Christian Medical Center (KCMC) ambayo imekuwa ikipata ufadhili wa shirika la EGPAF kupitia ufadhili wa Serikali ya watu wa Marekani tangu mwaka 2004, ambapo walifurahishwa na kuvutiwa na huduma zinazotolewa katika hospitali hiyo kwa kushirikiana na shirika la EGPAF.

Miongoni mwa huduma hizo ni mpango wa kuzuia maambukizi ya VVU kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto (PMTCT), huduma za matibabu na matunzo kwa watu wanaoishi na virusi vya UKIMWI na kusaidia huduma za maabara.
Pamoja na hayo EGPAF imeweza kujengea uwezo watoa huduma wa afya katika hospitali ya KCMC na kusaidia upatikanaji wa huduma rafiki za kisaikolojia kwa vijana na watoto wanaoishi na VVU katika mkoa wa Kilimanjaro.