Habari tulizozipata hivi punde kutoka mji wa Didia uliopo katika wilaya ya Shinyanga mkoani Shinyanga ni kwamba watu wanaodaiwa kuwa ni majambazi wamevamia duka la mfanyabiashara wa MPESA anayejulikana kwa jina la Emmanuel Mabutu.
Tukio hilo limetokea majira ya saa mbili/kuelekea saa tatu usiku wakati mvua ikiendelea kunyesha.
Mashuhuda wa tukio hilo wameiambia Malunde1 blog kuwa watu hao zaidi ya wawili wakiwa na bunduki na silaha za jadi yakiwemo mapanga wamevamia duka hilo kisha kuwaamuru wateja waliokuwa wamejazana ndani ya duka hilo wakipatiwa huduma,kutoka nje kisha kumwamuru Emmanuel kutoa pesa zinazodaiwa kuwa zaidi ya milioni 10 ,simu na vocha za simu ambazo thamani yake bado haijajulikana.
"Majambazi walikuwa wamevaa makoti,walipofika dukani waliwaamuru wateja watoke nje ya duka wakisema wanamdai pesa mwenye duka..wanataka wazungumze naye...ndipo wakamwamuru atoe pesa...kisha kurusha risasi hewani....baada ya muda mfupi ndipo Emma akatoka nje na kuanza kupiga kelele...."...wanasimulia mashuhuda wa tukio hilo.
"Huyu Emma ndiyo wakala mkubwa wa Mpesa hapa Didia...tunalaani kitendo hiki,tunaomba jeshi la polisi lifanye uchunguzi kuhusu tukio hili na kufanikisha kukamatwa kwa wahusika wa tukio hili",wamesema mashuhuda hao.
Baada ya kumaliza kufanya tukio hilo yalifyatua risasi hewani kisha kutokomea kusikojulikana na kwamba hakuna mtu aliyejeruhiwa katika tukio hilo.
SOMA HABARI KAMILI HAPA
Baada ya kumaliza kufanya tukio hilo yalifyatua risasi hewani kisha kutokomea kusikojulikana na kwamba hakuna mtu aliyejeruhiwa katika tukio hilo.
SOMA HABARI KAMILI HAPA