Baada bweni moja kuungua siku chache zilizopita, leo moto umelipuka tena shule ya Sekondari Iyunga mkoani Mbeya umeteketeza mabweni katika shule hiyo hadi sasa.
Bweni la Shaban Robert Inaelezwa kuwa mpaka sasa bweni la Shaban Robert linateketea na inaelezwa kuwa hakuna uwezekano wa kuokoa mali zilizomo ndani na bweni jingine limeanza kushika moto.
Chanzo cha moto huo bado hakijajulikana na juhudi za uokoaji zinaendelea.
Tukio hili limetokea wakati wanafunzi wakiwa darasani wakiendelea na masomo.
Ni mara ya pili sasa shule hiyo ya Iyunga kukumbwa na janga la moto
Social Plugin