Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amefanya uteuzi wa wakuu wa Mikoa 26 ya Tanzania Bara, ambapo kati yao 13 ni wapya, 7 wamebakizwa katika vituo vyao vya kazi, 5 wamehamishwa vituo vya kazi na 1 amepangiwa Mkoa Mpya wa Songwe.
Uteuzi huo umetangazwa na Kaimu Katibu Mkuu Kiongozi, Mhandisi Mussa Ibrahim Iyombe leo tarehe 13 Machi, 2016 Ikulu Jijini Dar es salaam.
- Mh. Paul Makonda - Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam.
- Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Elias Kyunga - Mkuu wa Mkoa wa Geita.
- Meja Jenerali Mstaafu Salum Mustafa Kijuu - Mkuu wa Mkoa wa Kagera.
- Meja Jenerali Mstaafu Raphael Muhuga - Mkuu wa Mkoa wa Katavi.
- Brigedia Jeneral Mstaafu Emmanuel Maganga - Mkuu wa Mkoa wa Kigoma.
- Mh. Godfrey Zambi - Mkuu wa Mkoa wa Lindi.
- Dkt. Steven Kebwe - Mkuu wa Mkoa wa Morogoro.
- Kamishna Mstaafu wa Polisi Zerote Steven - Mkuu wa Mkoa wa Rukwa.
- Mh. Anna Malecela Kilango - Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.
- Mhandisi Methew Mtigumwe - Mkuu wa Mkoa wa Singida.
- Mh. Antony Mataka - Mkuu wa Mkoa wa Simiyu.
- Mh. Aggrey Mwanri - Mkuu wa Mkoa wa Tabora.
- Mh. Martine Shigela - Mkuu wa Mkoa wa Tanga.
- Mh. Jordan Mungire Rugimbana - Mkuu wa Mkoa Dodoma.
- Mh. Said Meck Sadick - Mkuu wa Mkoa Kilimanjaro.
- Mh. Magesa Mulongo - Mkuu wa Mkoa Mara.
- Mh. Amos Gabriel Makalla - Mkuu wa Mkoa Mbeya.
- Mh. John Vianey Mongella - Mkuu wa Mkoa Mwanza.
- Mh. Daudi Felix Ntibenda - Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
- Mh. Amina Juma Masenza - Mkuu wa Mkoa wa Iringa.
- Mh. Joel Nkaya Bendera - Mkuu wa Mkoa wa Manyara.
- Mh. Halima Omary Dendegu - Mkuu wa Mkoa wa Mtwara.
- Dkt. Rehema Nchimbi - Mkuu wa Mkoa wa Njombe.
- Mhandisi Evarist Ndikilo - Mkuu wa Mkoa wa Pwani.
- Mh. Said Thabit Mwambungu - Mkuu wa Mkoa Ruvuma.
- Luteni Mstaafu Chiku Galawa - Mkuu wa Mkoa wa Songwe (Mkoa mpya).
Wakuu wote wa Mikoa walioteuliwa, wataapishwa Jumanne tarehe 15 Machi, 2016 saa 3:30 Asubuhi Ikulu, Jijini Dar es salaam.
Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
13 Machi, 2016
Unaweza tazama video ya uteuzi hapa
Social Plugin