Anaitwa Athanas Phabian a.k.a Dj hunter ni mtangazaji na mwandishi wa habari kwa miaka kadhaa toka alipohitimu chuo cha uandishi cha jijini Dar es salaam mwaka 2009.
Mpaka sasa ametimiza ndoto yake ya kuwa Dj wa kimataifa
kwenye kituo kimoja nchini Ujeruman radio Leinehertz.
Tofauti na kazi ya Udj jamaa
anapiga kazi mgodini.
Alizaliwa tarehe kama ya leo Machi 13 huko Singida Miaka Kibao iliyopita.
Ni miongoni mwa Madj wasiopenda sifa ila anaonekana
kulingana na ubunifu wake na bidii anazofanya radio alizopita ni Chuchu
fm Zanzibar 2010 ,Radio Faraja Fm ya Shinyanga mwaka 2012~2015.
Hivi sasa ni mshirika
wa radio ya kimataifa ya nchini Ujerumani akifanya kipindi cha Bongo
106.5 akiwa na Veronica Natalis.
Dj Hunter ni miongoni mwa wadau muhimu wa Malunde blog,ndiyo miongoni mwa watu waliochangia blog hii kujulikana kimataifa na pia ndiyo anajua siri ya blog hii kuitwa Malunde1 blog
Happy Birthday brother Dj Hunter!!!
Hizi hapa ni baadhi tu ya picha zake
Social Plugin