Najua mtu wangu wa nguvu unatamani kujua ni miji gani gharama zake za kuishi ni nafuu zaidi na pia ni ipi yenye gharama kubwa zaidi kuishi.
Economist Intelligence Unit wamefanya utafiti kuhusiana na Miji mikubwa Duniani yenye gharama kubwa zaidi za kuishi kwa mwaka 2016. Utafiti huu ulijikita zaidi katika kufanya mahesabu kwa kulinganisha bei za vitu mbalimbali kwenye miji 133, Mji wa Singapore umeshika namba moja kwa kuwa mji wenye gharama kubwa zaidi za kuishi.
Mji mkuu wa Zambia Lusaka kutoka Afrika ndio mji wenye gharama ndogo za kuishi Duniani, umechukua nafasi ya 133 ikiwa ni nafasi ya mwisho kwenye miji iliyofanyiwa utafiti ikifuatiwa na miji ya India Bangalore na Mumbai.
1.Singapore
2.Zurich-Switzerland
3.Hongkong
4.Geneva
5.Paris
6.London
7.New York
8.Copenhagen, Denmark
9.Seoul-South Korea
10.Los Angeles
133.Lusaka -Zambia