Ikiwa zimepita wiki mbili tangu kutokea kwa ajali Kimara Dar es salaam, Usiku wa kuamkia March 25 kumetokea ajali nyingine Kimara Baruti ambapo basi la Princes Muro lenye usajili namba T 551 BQP limevamia kituo kipya cha abiria.
Taarifa rasmi zinasema kuwa basi hilo lilokuwa likitokea Arusha kwenda Dar es salaam halikuwa na abiria wala hakuna aliyefariki, kwa mujibu wa muhusika wa basi hilo alisema wakati basi hilo lilipopata itilafu maeneo ya mto Wami wahusika walichukua uamuzi wa kuwaamisha abiria wote kutoka kwenye basi hilo na kuwapeleka kwenye basi lingine kwahiyo mpaka linaingia Dar na kupata ajali halikuwa na abiria.
Social Plugin