Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

KUTANA NA VERONICA NATALIS, MREMBO MWANAHABARI MWENYE NDOTO ZA KUMILIKI RADIO




Kuelekea siku ya wanawake Duniani ambayo huadhimishwa kila mwaka tarehe 08,Machi,Malunde1 blog imefanya mazungumzo mafupi na Mwanadada Veronica Natalis,ni mwandishi wa habari/anawakilisha Radio DW  pia mtangazaji katika Kituo cha Matangazo cha Radio Faraja Fm Stereo cha mjini Shinyanga.

Veronica Natalis ni mwanamke jasiri, anayejituma katika kazi bila kujali yupo katika mazingira yapi na furaha yake ni pale tu jambo alilokusudia kufanya linafanikiwa.
Baada ya kufanya kazi kwa muda katika vyombo vya habari kwa kuajiriwa na vingine kufanya kwa kujitolea sasa mrembo huyu ana ndoto ya Kumiliki Chombo chake cha Habari,kipaumbele kikiwa ni kumiliki Radio.
 
Anasema Malengo yake ni Kusaidia makundi ya watoto yatima, wajane na watu maskini.

“Machafuko mengi yanayotokea katika nchi za Afrika hasa zile zilizo kusini mwa jangwa la Sahara waathirika wakubwa wanakuwa ni wanawake, watoto na watu maskini” ,anasema Veronica.

Na hiyo ndiyo sababu kubwa inayomfanya aamini kuwa hayo ni makundi maalumu ambayo yanatakiwa kupewa msaada wa uhakika na kila mmoja analo jukumu hilo vikiwepo vyombo vya habari.

Veronica ambaye kwa sasa anafanya kazi na Radio Faraja iliyopo Shinyanga Tanzania na mwakilishi wa idhaa ya Kiswahili ya Radio DW iliyopo Bonn Ujerumani ,anasema vyombo vya habari vina majukumu makubwa ya kufikia makundi hayo ambayo kwa kiasi kikubwa yamesahaulika huku akiongeza kuwa hata katika maandiko matakatifu yanaelekeza kuwajali kwa ukaribu Yatima, wajane na watu maskini.

“Nchi za Afrika kama zitatengeneza mifumo mizuri itakayoyawezesha makundi hayo kuwa na maisha bora ni dhahiri kuwa mifumo kandamizi kwa wajane hasa ile ya mila na desturi itaondoka, watoto yatima watapata haki zao na hata watu maskini wataweza kuyafurahia maisha.

KUHUSU RADIO ZA KIMATAIFA.

“Ni ndoto ambayo pia niliishi nayo kwa muda mrefu tangu nikiwa nasoma shule ya msingi nilikuwa nikisikiliza DW/ VOA na BBC na nikasema ipo siku nitafanya kazi na radio hizo”Alisema Natalis.

Anaamini kuwa kufanya kazi na radio za kimataifa kunamsaidia mwandishi kupanuka hata mawazo anayowaza yanakuwa ya kimataifa.

“Unajua karibu matatizo ya nchi za Afrika yanafanana ,sasa hiyo inakuwa ni fursa nzuri ya kutatua matatizo ya watu kupitia vyombo vya habari ,unaweza kuwa ni mwandishi unaishi Tanzania lakini ukasaidia jamii ya Congo Burundi, Ghana na kwingineko…..

….Napenda sana kutengeneza vipindi vya radio, napenda kuzifikia jamii zilizo pembezoni kabisa nikiamini na hiyo ndio furaha ninayoipata katika kazi yangu. Siku moja naamini nitamiliki radio ili niendeleze harakati za kuwasaidia watanzania na wasio watanzania hasa makundi ya Yatima, Wajane na Maskini”,anasema.
Nimekuwekea picha za Veronica Natalis hapa chini akiwa katika mazingira mbalimbali....Je Ndoto zake zitatimia???
 Natalis.
Veronica Natalis akiwajibika Radio Faraja

































Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com