Habari Mpya

6/recent/ticker-posts

Majanga Shinyanga!! MVUA YAUA MTOTO KANISANI,YAJERUHI WAFAIDIKA 10 WA TASAF


Mtoto aliyejulikana kwa jina la Ibrahim Elias mwenye umri wa miezi mine amefariki dunia baada ya kuangukiwa na paa la kanisa la Waadventista Wasabato(SDA)wakati mvua ikinyesha katika kijiji cha Luhaga kata ya Igwamanoni wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga.


Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari,kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Dismas Kisusi alisema tukio hilo limetokea jana saa 8:30 katika kijiji hicho.


Alisema kutokana na mvua iliyokuwa inanyesha paa la kanisa la SDA lilimwangua mtoto huyo na kusababisha kifo chake na kujeruhi watu kumi ambao ni wafaidika wa mfuko wa maendeleo ya jamii(TASAF) waliokuwa wamekusanyika kwa ajili ya kupata msaada.


Aliwataja majeruhi katika tukio hilo kuwa ni Madelena Muhangwa(60),Elizabeth Ngasa(50),Milembe Magembe(43),Lucia James(42) na Mary Lazima(28 .
 
Wengine waliojeruhiwa ni Siwema Ndayamawe(miezi 9),Leticia Masasila(50),Malosha Kakoja(60),Esther Bufumbe(30) na Esteria Marco(28).


Kamanda Kisusi alisema majeruhi wote ni wakazi wa kijiji cha Luhaga kata ya Igwamanoni wilayani Kahama na walitibiwa katika kituo cha afya cha Igwamanoni na kuruhusiwa kurudi kwao.
Na Kadama Malunde-Malunde1 blog

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com