Brigit akiwa na nguo alizoiba
Suruali za ndani na soksi zilizoibwa na Brigit
Paka mmoja mwizi wakati wa usiku amekuwa akiiba soksi pamoja na nguo za ndani nchini New Zealand.
Katika kipindi cha miezi miwili, paka huyo mwenye umri wa miaka sita kwa jina Brigit kutoka mji wa Hamilton aliiba suruali za ndani 11 na zaidi ya soksi 50.
Mmiliki wake Sarah Nathan alichapisha tabia ya paka huyo isiyo ya kawaida katika mtandao wake wa facebook.
''Tabia hiyo sasa inazidi kuwa mbaya.Lazima kuna mtu ambaye anakosa vitu vyake'',alisema katika chapisho lake la ukursa wa facebook lililosambazwa mara 500.
Bi Nathan ameimbia BBC kwamba tatizo lilianza alipogundua vipande kadhaa vya nguo za ndani katika nguo zake anapoziosha.
''Suruali hizo za ndani hazikuwa zetu,na siku moja Brigit aliingia katika chumba cha wageni akiwa amebeba soksi aliongezea'',akisema kuwa waathiriwa wa Brigit walikuwa majirani katika nyumba za ghorofa.
Chanzo-BBC
Social Plugin