Aliyewahi kuwa Mbunge wa Same Mashariki ambaye kwa sasa ni Mkuu wa Mkoa mteule wa Shinyanga, Anna Kilango Malechela, amesema jitihada zake na utendaji katika kuihudumia jamii ndio sababu kuu iliyomfanya Rais Magufuli kumpa nafasi ya kuuongoza mkoa wa Shinyanga.
Akizungumza kupitia Kipindi cha Sun Rise cha Times Fm, Malechela amedai hata ‘anguko’ lake katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana, aliangushwa na watu wenye sababu binafsi na si kukataliwa na Wananchi.
“Mungu ni mwema, sikuwa na hili wala lile, nimekaa Bungeni miaka 15 na Mh Rais akiwa kama Mbunge, kwahiyo alikuwa anaona utendaji wangu, kupambana na kero za wananchi na jinsi nilivyo na jitihada.
“Unajua wanaosema tunabebwa tulianguka kwenye uchaguzi, watazame kwa upana zaidi, wengine tuliangushwa, naahidi kutumia kauli mbiu ya kazi tu kuitumikia Shinyanga” Alisema Mama Anna Kilango.
Social Plugin