Mwanamme aliyejulikana kwa jina la Moshi Saliboko(36) mlinzi na mkazi wa kijiji na kata ya Isaka wilayani Kahama mkoani Shinyanga ameuawa kwa kunyongwa shingo na miguu yake kufungwa kamba umbali wa mita 15 kutoka lindoni kwake katika kampuni ya simu ya Zantel.
Kwa mujibu wa kaimu kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Dismas Kisusi amesema marehemu aligundulika kuuawa Machi 28,2016 ,majira ya saa 1:00 asubuhi katika kitongoji cha Majengo,kijiji cha Isaka Station kata ya Isaka wilaya ya Kahama.
Amesema mlinzi huyo Moshi Saliboko aliuawa kwa kunyongwa huku miguu yake ikiwa imefungwa kamba kisha wauaji kupora vipande vine vya Battery Backup,Rada Type 165AH,1PG Battery na 3CUWENT Transformer na wauaji hao kutokomea kusikojulikana.
Amesema chanzo cha tukio hilo ni kuwania mali na kwamba jeshi la polisi linafanya msako kuwabaini na kuwakamata wahusika wa tukio hilo.
Na Kadama Malunde-Malunde1 blog
Social Plugin