Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk Ali Mohammed Shein amemteua
Balozi Seif Ali Idd kuwa Makamu wa Pili wa Rais wa visiwa hivyo.
Kwa
mujibu wa mamlaka aliyopewa chini ya kifungu cha 39 (2) cha Katiba ya
Zanzibar ya mwaka 1984, Dk Shein amemteua Balozi Idd ambaye alikuwa na
wadhifa huo hata kipindi kilichopita.
Uteuzi
wa Balozi Idd aliyezaliwa Februari 23, mwaka 1942, ulianza jana ikiwa
ni siku nne tangu kuapishwa kwa Shein kuwa Rais wa Zanzibar.
Balozi
Idd anakuwa mtu wa pili kuteuliwa na Dk Shein baada ya kuteuliwa kwa
mwanasheria mkuu wa Zanzibar Said Hassan Said mwishoni mwa wiki.
Dk
Shein sasa atakuwa na wakati mgumu wa ama kumteua au kutomteua Makamu
wa Kwanza wa Rais ili kukidhi matakwa ya Serikali ya Umoja wa Kitaifa
(SUK) kwani hakuna chama cha upinzani kilichokidhi vigezo vya kushirikishwa katika kuunda Serikali.
Social Plugin