TAARIFA YA JESHI LA POLISI KUHUSU AJALI YA MAGARI MAWILI HUKO SINGIDA





JESHI LA POLISI TANZANIA OFISI YA KAMANDA WA POLISI “M” SINGIDA 10.03.2016 TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI (PRESS RELEASE) AJALI YA MAGARI MAWILI KUGONGANA NA KUSABABISHA MAJERUHI,KIFO NA UHARIBIFU.
 Mnamo tarehe 09.03.2016 majira ya saa 9:30 alasiri huko katika maeneo ya Mnung’una, Kata ya Msisi , Wilaya na Mkoa wa Singida, Barabara ya Singida – Nzega , Gari lenye namba za usajiri T. 261 AMX MITSUBISH FUSO BASI mali ya Kampuni ya Kandahari ikiendeshwa na Dereva aitwaye Noshard s/o Rajabu, (24), Mchaga na mkazi wa Arusha akitokea Arusha kwenda kiomboi aligongana na Gari yenye namba T.344 BRZ/T.422 BGN SCANIA TANKER mali ya OLYMPIC PETROLIUM – MWANZA ikiendeshwa na Dereva aitwaye Yusuph s/o Magori, (58), Mzanaki mkazi wa Vingunguti – Dar es salaam akitokea Tabora – Dar es salaam na kusababisha kifo Nasuela s/o Nsaning’o, (80), Mkulima na mkazi wa Kiomboi - Singida aliyekuwa abiria katika BASI na mejeruhi kwa watu saba na uharibifu wa magari hayo.
 Aidha waliopata majeraha sehemu mbalimbali za miili yao katia ajali hiyo ni pamoja na Noshard s/o Rajabu, Dereva wa BASI, Yusuph s/o Magori, Dereva wa SCANIA TANKER na Elias s/o Yusuph, (23) Utingo wa SCANIA TANKER mkazi wa Vingunguti – Dar es salaam. 
Wengine ni abiria wa BASI ambao ni Recho d/o Benjamini, (38), Mnyiramba, mfanyabiashara na Makzi wa Buguruni – Dar e salaam, Kefas s/o Marko, (23), mkulima na mkazi wa Kiomboi – Singida, Ramadhani s/o Hamis, (26), Mkulima na mkazi wa Babati – Arusha na Ruti d/o Nasuela, (42), Mkulima na mkazi wa Kiomboi .
Chanzo cha ajali hiyo kimebainika kuwa ni mwendokasi wa dereva wa BASI ambapo alishindwa kulimudu na kuhamia upende usiokuwa wake na kulifuata Gari lililokuwa linakuja mbele yake. Majeruhi wote wamepelekwa katika Hospitali ya Mkoa Singida kwa matibabu na hali zao zinaendelea vizuroi na Dereva wa Basi Noshard s/o Rajabu anashikiliwa na Jeshi la Polisi kwa mahojiano na baada ya mahojiano kukamilika atafikishwa mahakamani.
 Jeshi la Plosi linatoa wito kwa madereva wote wa vyombo vya usafirishaji kuendesha vyombo vyao kwa kuzingatia kanuni,taratibu na Sheri za usalama barabarani. THOBIAS G.SEDOYEKA – ACP KAMANDA WA POLISI (M) SINGIDA

Download/Pakua/Install App ya Malunde 1 blog Google Playstore Bofya Hapa

Je, unayo taarifa ya kusisimua ambayo ungependa tuichapishe? Tafadhali, wasiliana nasi kupitia malundekadama@yahoo.com
Previous Post Next Post