Mamlaka ya chakula na dawa nchini TFDA kwa kushirikiana na jeshi la Polisi wamegundua na kukifungia kiwanda bubu cha kutengenezea vipodozi bandia jamii ya manukato eneo la Tuangoma Kigamboni nyumbani kwa mtu na kumshikilia mmliki wa nyumba hiyo kwa mahojiano zaidi.
Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya chakula na dawa nchini TFDA Bw. Hiiti Silo pamoja na kuainisha bidhaa hizo kuwa hatari kwa afya za binadamu amesema hatua hiyo inafuatiwa kukamatwa kwa maduka ya mfanya biashara mmoja eneo la sinza jijini Dar es Salaam akiwa na shehena ya bidhaa hizo zenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni mia moja zikiwa na vifungashio vya kuzalishwa nchini uturuki.
Aidha katika heka heka za maofisa wa TFDA na Polisi kukamatwa kiwanda hicho mmiliki wa nyumba hiyo aligoma kuongea lolote kuhusu uzalishaji bidhaa hizo kabla ya kubebwa na kupelekwa polisi kwa mahojiano.
Via>>ITV
Social Plugin