Taasisi ya Mo Dewji Foundation wakishirikiana na kampuni ya Darecha Limited wametangaza majina ya washiriki 20 bora wa shindano la Mo Mjasiriamali (Mo Entrepreneurs Competition). Shindano la Mo Mjasiriamali lilizinduliwa mwezi wa Januari, 2016 na mkurugenzi mtendaji wa makampuni ya MeTL na mwenyekiti wa Mo Dewji Foundation, Bilionea Mohammed Dewji. Akizindua shindano hilo mweneyekiti huyo alisema,
"Tatizo la ukosefu wa mitaji ni kikwazo kikubwa kwenye ukuaji wa biashara za vijana wengi hapa nchini.Hivyo ni muhimu kuwaongezea vijana fursa za upatikanaji wa mitaji"
Shindano la Mo Mjasiriamali linalenga kuwainua vijana wenye shauku, ari na nia ya dhati ya kukuza biashara zao ili kujiongezea kipato na mchango wao katika ujenzi na ukuaji wa uchumi wa Tanzania.
Wakitangaza majina ya washiriki 20 bora, waratibu wa shindano la Mo Mjasiriamali wamesema shindano hili limewafikia maelfu ya vijana katika maeneo mbali mbali ya Tanzania. Vijana wapatao 200 wanaomiliki biashara changa walituma maombi ya ushiriki. Washiriki waliotuma maombi walikuwa na wastani wa umri wa miaka 26, miongoni mwao asilimia 13 ni wa jinsia ya kike. Aina mbalimbali za biashara kama vile, biashara za kilimo, ufugaji, utengenezaji wa mbolea, tehama na nishati zilionekana kupata washirki wengi zaidi.
Majina ya washiriki 20 watakaofanyiwa usaili na jopo la majaji litakaloongozwa na mwenyekiti wa Mo Dewji Foundation, Ndg. Mohammed Dewji, majina ya biashara zao na mkoa wanaotoka kwenye mabano, ni:
1.Edgar Mwampinge (Spid Express Courier&Logistics, DSM),.
2.Geofrey Boniphace (Brain Bongo Media Network, DSM),
3.Alexander Jokoniah (Mazimbu Agro Enterprises,Morogoro),
4.Raphael Malongo( Malongo Poultry Farm,Singida),
5.Sirjeff Khagolla (Jefren Agrifriend, DSM),
6.Erick Karoli (Tado Travel, Arusha),
7.Ahad Katera (Guavay, DSM),
8.Bonkey Kaigembe (Igale Company, Mbeya),
9.Gerald Reuben(Nitume Sokoni, Pwani),
10.Selenga Kaduma(Agro Forest, Njombe),
11.Saturnin Tarimo (Galaxy Energy Solutions, DSM),
12.Ally Msigwa (Alishati Investments,Iringa),
13.Khadija Liganga (Dida Vitenge Wear, Mwanza),
14.Williard Kaaya (Newhope Cassava Flour, DSM),
15.Doreen Assey (Dee Bakery,DSM),
16.Clemence Makoyola(Easternwind Investment, Morogoro),
17.Emmanuel Ngalewa( Ngama Technologies, DSM),
18.Eric Mutta (Problem Solved, DSM),
19.Francis Saanane( Hub Networks, DSM),
20.Fredrick Swai (Nact Technology Hub, Mbeya)
Washiriki wote ishirini watafanyiwa usaili wa kina kuhusu biashara zao ambapo miongoni mwao watapatikana washindi watatu(3) hadi watano(5). Washindi hao watatangazwa siku ya tarehe 19 Aprili na kupatiwa kiasi cha milioni shilingi milioni 10 kila mmoja ili kukuza biashara zao.Pia washindi hawa watakuwa wakikutana na mkurugenzi mtendaji wa MeTL na mwenyekiti wa Mo Dewji Foundation kwa ushauri kuhusu namna ya kukuza biashara zao.
Kwa maelezo zaidi tembelea: http://www.modewjifoundation.org/mo-entrepreneurs-competition/
Social Plugin